TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, November 13, 2012

LIONEL MESSI AITIKISA SAUDI ARABIA

 























RIYADH, Saudi Arabia
Kulikuwa na vurugu zisizokuwa za kawaida kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mfalme Khaled jijini Riyadh baada ya kuwasili kwa kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kujiandaa na mechi yao ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Saudi Arabia kwenye Uwanja wa Mfalme Fahd kesho Jumatano.

Maafisa wa Uwaja wa Ndege walilalamikia kitendo cha maelfu ya mashabiki kufika uwanjani na kulazimisha wapewe nafasi ya kumuona nyota wa Argentina na klabu ya Barcelona ya Hispania, Lionel Messi.

Licha ya ulinzi mkali wa polisi waliokuwa na silaha za moto kwenye uwanja wa ndege na pia katika barabara nzima ya kuelekea uwanjani, bado mamia ya mashabiki wa Messi walifanikiwa kupenya na kufika uwanjani.

Straika huyo alifika jijini Riyadh kwa ndege yake binafsi pamoja na familia yake kabla ya kuwasili kwa wachezaji wengine.

Hata hivyo, askari kibao waliokuwa uwanjani walitumia 'akili' za ziada kuwapiga chenga mashabiki na kufanikiwa kumuondoa Messi uwanjani.

Mashabiki wengi na maafisa wa usalama walilaumu vurugu za kulazimisha kumuona Messi kweny uwanja wa ndege, wakisema kwamba ishara hiyo si nzuri kwa timu ya taifa ya Saudi.

Waandishi wa habari pia walikuwa na kazi kubwa ya kuripoti tukio la ujio wa Messi na wenzake kwani walizuiwa kuwapo kwenye ukumbi ambao wachezaji walikusanyika.

No comments:

Post a Comment