UHABA WA NISHATI YA MAFUTA WALETA GUMZO BUNGENI
  | 
| Mbunge wa Ubungo John Mnyika akiwasilisha hoja inayohusu  uhaba wa mafuta Bungeni | 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda (aliyesimama) akijibu hoja ya Mh. John Mnyika.
 
Na Mwandishi wetu, Dodoma.
 
Mbunge
 wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika akihoji kiti cha spika juu ya serikali 
kushindwa kuleta bungeni kauli ya serikali juu ya mkakati wa serikali 
kukabiliana na uhaba wa mafuta nchini Tanzania.
Uhaba
 wa mafuta leo umewakimbiza kwenye kikao cha bunge mjini Dodoma asubuhi,
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na naibu mawaziri
 wake George Simbachawene na Steven Masele.
Waziri
 huyo na naibu mawaziri wake hawakuwepo bungeni leo wakati Mbunge wa 
Ubungo (CHADEMA) John Mnyika alitaka serikali itoe sababu ya kutokuja 
bungeni leo kutoa tamko la serikali ya jinsi inavyoshughulikia swala la 
uhaba wa mafuta nchini.
Spika
 wa Bunge Anne Makinda alimlazimisha Waziri kuu Mizengo Pinda kusimama 
na kujibu hoja ya Mnyika aliyemtaka Spika kulazimisha serikali ijibu 
hoja  yake pamoja na mkakati wa serikali wa kutatua uhaba wa mafuta 
nchini.
Waziri
 Mkuu  Mizengo Pinda alilazimika kunyanyuka nakusema kwa ufupi kuwa 
serikali ilikuwa ikijiandaa na kuja na hoja nzito ya kueleza umma 
mikakati kabambe ya kutatua uhaba wa mafuta nchini.
 
No comments:
Post a Comment