TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Friday, November 2, 2012

ALLY KIBA,ASLAY NA SAIDA KAROL WATAJWA KUWANIA TUZO ZA KORA 2012

























Baada ya kukaa kwa muda hatimaye majina ya wasanii watakaowania tuzo za Kora za mwaka huu yametoka. Tuzo hizo za mwaka huu zitakuwa na ugeni mkubwa wa Chris Brown.
Ali Kiba ametajwa kuwania kwenye kipengele cha Best Male East Africa kwa wimbo wake Single Boy aliomshirikisha Lady Jaydee. Ali Kiba atachuana na Jimmie Gait Feat Dk – Furi Furi Dance, Kenya,Kidum Feat Sana – Mulika Mwizi, Burundi, Redsan – Ila Wewe, Kenya, Chris D – Aisha, Burundi na Mulatu Astatke – Ethiopie, Ethiopia.

Aslay ametajwa kwenye kipengele cha Best Male Newcomer na wimbo wake Niwe Nawe akipambana na Floby – Saanida, Burkina Faso, Loyiso – Wrong To You, Afrique Du Sud, Aziz Azion – My Oxygen, Uganda, Davido – Dami Duro, Nigeria, John Chiti – Wapusuku, Zambie.

Naye Saida Karoli anawania kipengele cha Best Female East Africa kwa wimbo wake Sakina ambapo anachuana na Juliana Kanyomozi – I Am Ugandan, Marya – Shiki Simu, Kenya, Helen Berhe – Lebe, Ethiopia, Asther Aweke – Lu Mili, Ethiopia na Ikraan Caraale – Gaarsiiya, Somalia.

Tuzo hizo zitafanyika December 29 nchini Ivory Coast.

No comments:

Post a Comment