BALOZI PETER KALLAGHE AKUTANA NA MAAFISA WA BODI TA UTALII TTB
![]()  | 
| Mhe.Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe | 
Mh.Balozi wa Tanzania nchini 
Uingereza  Balozi Peter Kallaghe leo ameitisha mkutano kati yake na 
maafisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na maafisa wa Ubalozi ili 
kuzungumza nao na  kupata taarifa muhimu  juu ya maadandalizi ya 
ushiriki wa Tanzania katika maonyesho ya utalii ya (WTM),  
yanayotarajiwa kuanza siku ya jumatatu Novema 5 mpaka Novemba 8 mwaka 
huu katika jiji la London.
Maonyesho ya Utalii ya (WTM)  yanayoandaliwa nchini Uingereza ni
 maonyesho makubwa  na yanashirikisha makampuni kutoka mataifa 
mbalimbali duniani kwa ajili ya kuuza bidhaa zao, hasa Mahoteli, 
Makampuni ya Ndege na makampuni ya Utalii, Mwaka huu Tanzania 
inashirikisha makampuni zaidi ya 55 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.
Katika picha juu akisisitiza 
jambo katika mkutano huo, wakati wa mkutano huo ambapo aliza kila jambo 
ambalo linahitaji kupata majwabu muhimu kabla ya kuanza kwa maonyesho 
hayo.


No comments:
Post a Comment