POLISI AFUKUZWA KAZI BAADA YA KUMBAKA MTUHUMIWA WA KIKE
JESHI la Polisi mkoani Mbeya limemfukuza kazi askari wake Enock  Daffa 
(22) kwa tuhuma za kufanya  mapenzi na mtuhumiwa wa kike mwenye  umri wa
 miaka 25 katika Kituo cha Polisi cha Mji mdogo wa Tunduma,  Wilaya ya 
Momba, mkoani hapa. 
Kwa mujibu 
wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,  Athuman Diwani, askari huyo 
alitenda kosa hilo Novemba 21,2012 na kwamba  mtuhumiwa aliyefanya naye 
mapenzi alikuwa akikabiliwa na kosa la wizi.
Kamanda Athumani 
alisema kuwa mbali ya kufukuzwa  kazi askari huyo tayari amefikishwa 
katika Mahakama ya Wilaya ya Mbozi  ili sheria iweze kuchukua mkondo 
wake.
Aidha alisema kuwa hali kama hiyo haitaweza kuvumiliwa na Jeshi la Polisi na kwamba atakayebainika kufanya tukio kama hilo adhabu yake itakuwa ni kufukuzwa kazi.
Kamanda huyo alitoa wito kwa 
askari polisi kufanya  kazi kwa kufuata sheria na kanuni za Jeshi la 
Polisi kama mwongozo  unavyowaagiza ili kulinda maadili ya Jeshi la 
Polisi ambacho ndicho  chombo kinachotumika na wananchi katika 
kuzisimamia sheria.
Akizungumzia tukio hilo, baba mzazi wa 
askari huyo  alisema kuwa kitendo alichofaya mtoto wake si cha kiungwana
 ambacho pia  kimetia fedheha familia yake pia kwa jeshi la Polisi 
ambalo limepewa  dhamana ya kutunza usalama wa raia na mali zake.

No comments:
Post a Comment