VIONGOZI WA DINI WAKUTANA ARUSHA KWA AJILI YA KUOMBA AMANI KWA NCHI ZA EAC
NA: GLADNESS MUSHI - ARUSHA
Viongozi
wa dini wakiwemo wachungaji zaidi ya 400 kutoka katika nchi za Jumuiya
ya Afrika ya Mashariki wamekutana Jijini Arusha katika Kongamano kwa
ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya uongozi wao pamoja na kuombea nchi
hizo amani hasa ya Nchi ya Kenya na Tanzania. Akiongea na “FULLSHANGWE”
jana mratibu wa kongamano hilo ambalo limeandaliwa na mtandao wa
wachungaji mkoa wa Arusha,alisema kuwa kongamano hilo lina manufaa
makubwa sana kwa
Nchi hizo
Ayo
alisema kuwa amani ya nchi inatakiwa ipite hata kwa viongozi wa dini
kwa kuwa wao wana nafasin kubwa sana ya kuweza kuhubiri amani tofauti na
viongozi wengine wowote hivyo basi mtandao huo umechukua nafasi hiyo
kwa ajili ya kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakuwa na amani
Alisema
kuwa wachungaji hao zaidi ya 400 ambao wamekutana Jijini Arusha
wameweza kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na hata jinsi ya
kulinda amani ambayo baadhi ya Nchi imepotea kwa sababu mbalimbali hivyo
kupitia kwa waumini wao wataweza kuwafanya wananchi walinde amani
“Tumekutana
hapa kuhakikisha kuwa tunajadili mambo mbalimbali ya msingi lakini pia
kuhakikisha kuwa kila Kiongozi anakuwa balozi wa kulinda amani na wala
sio kwenye serikali kwani sisi Viongozi wa dini tuna nafasi kubwa sana
ya kutekeleza suala hilo ambalo wakati mwingine tunaachia Serikali
pekee’aliongeza Ayo
Mbali
na hayo aliwataka Viongozi wa dini kuhakikisha kuwa wanajiwekea
utaratibu wa kuhakikisha kuwa mbali na kuomba amani kwa nchi husika
lakini watumie nafasi mbalimbali ambazo wanazo kwa kuwataka waumini wao
waweze kufanya kazi kwa bidii na kisha kupambana na Umaskini
Alifafanua
kuwa kama Viongozi wa dini wataweza kufanya hivyo basi wataweza kuondoa
Mataifa ya jumuiya ya Afrika ya Mashariki hususan Tanzania kutoka
katika hali ya umaskini ambayo ipo na kufika katika viwango vya hali ya
juu ambapo hata hali ya ugumu wa maisha wakati mwingine inachangia sana
uharibifu wa amani, pamoja na umaskini.
“Kwa
sasa kuna changamoto kubwa sana za masuala ya kimaisha lakini viongozi
wa dini wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanaweka utaratibu wa kusisisitiza
watu wahakikishe kuwa wanafanya kazi na waache kukaa kaaa ovyo mitaani
na pindi wanapokaa mitaani ndipo wanapofanya na kuwaza hata mbinu za
kuharibu amani’aliongeza Ayo
No comments:
Post a Comment