WANAHABARI WATAKIWA KUFANYA UTAFITI WA KINA WANAPOANDIKA HABARI ZAO
Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar
Meneja
wa Baraza la Habari kanda ya Zanzibar Suleiman Seif Omar ( Bin Seif)
amewataka waandishi wa habari kufanya utafiti wa kina katika habari
wanazoziandika kama zina ukweli na uhakika. Hayo aliyasema jana wakati
akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali katika ukumbi
wa Mansoon Hotel Vuga Alisema
waandishi wa habari wanapokuwa kazini wawe makini kuandika habari
zinazozingatia maadili yote ya habari ikiwemo ukweli na uhakika.
Alisema kuandika habari kwa kuzingatia vigezo hivyo kunamuwezesha mwandishi kuwa muadilifu na kujiamini katika kazi yake.
Alisema
Baraza la Habari Tanzania kazi yake ni kushajihisha waandishi wa habari
na kuiwapa muongozo jinsi wa utafutaji wa habari na kuziandika vyema
ili ziwafikie wananchi wa taifa hilo .
“Kila
mtu ana haki ya kupata habari ila habari hizo ziwe za ukweli na uhakika
hivyo mwandishi nalazimika kuzifanyia utafiti wa kina habari
anazozipata kabla ya kuziwasilisha kwa wananchi kupitia chombo cha
habari”. Alisisitiza Bin Seif.
Meneja
huyo aliwaambia waandishi wa habari wawe watafiti wa habari na matukio
ili kuziwasilisha kwa wananchi kama tukio hilo lilivyotokea.
Nae
mwandishi wa BBC Ali Saleh (Alibato ) alisema kuwa waandishi wa habari
wanatakiwa kujifunza zaidi ili kuepukana na makosa ambayo hayastahiki
kujitokeza na kuitia aibu fani hiyo.
“Habari
zipo lakini waandishi wa habari hakuna kutokazana na kutoweza kujifunza
kusoma makala, vitabu pamoja kutosikiliza habari mbali mbali za ndani
na nje ya nchi”. Alisema Ali Saleh.
Nao
waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo walisema hakuna uhuru wa
kutosha katika kutoa habari jambo ambalo linawajengea hofu na
kutokujiamini katika kazi zao .
Mkutano
huo wa siku moja kwa Waandishi wa Habari umeandaliwa na Baraza la
Habari Tanzania (MCT) ambao umebeba mada Haki ya Kupata Habari
No comments:
Post a Comment