TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, March 18, 2013

LOWASA ASAIDIA KUKUSANYA SH. 85 MIL ZA AJIRA KWA VIJANA
photo5 5a214

Na: Happy Lazaro- Arusha.
Waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa amefanikisha kukusanywa kwa Sh85 milioni katika harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana, mkoani Arusha. Harambee hiyo iliyofanyika juzi, iliandaliwa na Umoja wa Waendesha Pikipiki (Uwapa) wa Jiji la Arusha. Akizungumza katika harambee hiyo, Lowasa ambaye pia

ni Mbunge wa Monduli, aliwataka vijana kujiepusha na ushawishi wa wanasiasa wanaowarubuni ili kushiriki katika maandamano yasiyokuwa na tija.
Badala yake, aliwataka wajikite katika kuzungumzia maendeleo yao. Alisema fedha zilizopatikana katika tukio hilo, ni vyema zikatumika katika kukopeshana ili kupanua mitaji ya biashara zao.

No comments:

Post a Comment