MSAFARA WA KINANA WATEMBELEA GUANZHOU
Mnara wa Canton wa mjini Guangzhou, China ambao una uregu wa zaidi ya mita 100.
Mtumishi katika mnara wa Canton, mrefu
kuliko yote nchini China na watatu duniani kwa urefu, Sarah Xie,
akimuonyesha mandhari ya jiji la Guangzhou, Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana, wakati Kinana na ujumbe wake walipopanda hadi mwisho
mnara huo wenye urefu wa zaidi ya futi 100, Machi 13, 2013. Wengine
Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na Katibu Mkuu wa
UVCCM, Martine shigella. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya
siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China
(CPC).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
na ujumbe wake wakitazama maumbo ya mandhari ya mji wa Guanzhou, China,
yaliyopo ndani ya mnara wa Cnton wenye urefu wa zaidi ya mita 100,
walipotembelea mnara huo, Machi 13, 2013. Kinana na ujumbe wake wapo
nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha
Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu wa NEC, Ushirikiano wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
mjini Magharibi, Yussuf Mohamed Yusuf wakitaza bidhaa zinazouzwa kwenye
kilele Mnara wa Canton ambao ni mrefu kuliko yote nchini China ukiwa na
urefu wa zaidi ya mita 100, mjini Guangzhou, China. Dk. Asha-Rose Migiro
na Yusuf ni miongoni mwa viongozi walioambatana na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana katika ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa
Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
akijaribu uzito wa spika, alipotembelea Kituo kikubwa cha Sayanasi na
Teknolojia cha Ljieafun cha Guangzhou, kinachojihusisha na ubunifu na
utengenezaji 'paisi' za sauti na uchanganyaji ragi na matangazo kama ya
biashara katika kumbi za muziki au vituo vya televisheni. Kulia ni Rais
wa Kituo hicho, Mike Fung na wapili kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa, CCM, Dk. Asha-Rose Migiro. Kinana na ujumbe wake
wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama
Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
akipewa zawadi na Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha
Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli
ya Exibition International mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013.
Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo
kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
akimpa vipeperushi kuhusu utalii wa Tanzania, Kamishna wa maadili na
nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui
Jian, kwenye hoteli ya Exibition International mjini Dongguan, China,
Machi 13, 2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi
ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana
akiwa katika mazungumzo na Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha
Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli
ya Exibition International mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013.
Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo
kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
akiwa na Kamishna wa Maadili wa CHama Cha Kikomunisti cha China, jijini
Dongguan, Cui Jian, katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na
Kamishna huyo, Machi 12, 2013. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Kinana na ujumbe wake wapo nchini
kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti
cha China (CPC).
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
akizungumza na Maofisa wa Mambo ya Nje wa Dongguan, China, Sarah Xie
(kulia) na Sabina Liu, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na
Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (PCP)
jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli ya Exibition International
mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013. Kinana na ujumbe wake wapo nchini
kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha
Kikomunisti cha China (CPC).
Katibu wa NEC, CCM, Siasa na Uhusiano
wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akizungumza na Maofiwa wa Mambo ya
Nje wa Dongguan Sarah Xie (kulia) na Sabina Liu, wakati wa chakula cha
jioni kilichoandaliwa na Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha
Kikomunisti cha China (PCP) jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli
ya Exibition International mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013.
Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo
kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC).
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar)
Vuai Ali Vuai, akizungumza na Maofiwa wa Mambo ya Nje wa Dongguan Sarah
Xie (kulia) na Sabina Liu, wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa
na Kamishna wa maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China
(PCP) jimbo la Dongguan, Cui Jian, kwenye hoteli ya Exibition
International mjini Dongguan, China, Machi 13, 2013.
Picha Juu na Chini Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na
wanachama wa Jumuia ya watanzania China.Picha na Bashir Nkromo-China
CHAMA Cha Kikomunisti cha China (CPC)
kimeeleza matumaini yake kwamba upo uwezekano wa Tanzania kupiga hatua
kubwa kichumi kama inajikita kwa dhati katika kuzitumia rasilimali
ilizonazo ikiwemo ardhi.
Hayo yalisemwa Machi 13, 2013 na
Kamishna wa Maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC),
jimbo la Donguan, China, Cuo Jian, wakati akizungumza na Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, katika hoteli ya Exhibition
Internation mjini hapa.
Jian ambaye pia ni Meya wa jiji la
Donguan, alisema, Tanzania kama zilivyo nchi kadhaa za Afrika, inaweza
kupiga hatua kiuchumi ikiwekeza juhudi zake katika kuzitumia rasilimali
ilizonazo kwa kuwa rasilimali ndiyo msingi wa kwanza katika kuinua
uchumi wa nchi yoyote.
Alisema, anatambuwa kwamba Tanzania ni
moja ya nchi za Afrika zenye ardhi kubwa, hivyo haina budi juhudi zake
za kuinua uchumi kuzielekeza katika rasilimali hiyo ikiitumia kwa kilimo
cha kisasa, kujenga viwanda na vitegauchumi mbalimbali ambavyo
vitachochea kukua haraka kwa uchumi.
"Hata hivyo nawapongeza Tanzania, kwa
hatua mliyofikia sasa katika kukuza uchumi, asilimia sita ya GDP,
inaridhisha, la msingi serikali kuongeza juhudi na kuwahamasisha
wananchi kushiriki katika juhudi hizo", alisema, Jian.
Akijibu swali na Mwenyekiti wa CCM
mkoa wa Simiyu, ambaye yupo kwenye msafara wa Kinana katika ziara hiyo,
Titus Kamani aliyetaka kujua ni nini hasa China ilifanya hadi kuufanya
uchumi wake ukue haraka na kuwa nchi ya pili dunia kwa maendeleo, Jian
alisema, China imefikia mafanikio hayo kutokana na kuamua kuwekeza kwa
nguvu zake zote kwenye rasilimali ya ardhi.
"Zipo njia nyingi za kuweza kuinua
uchumi wa nchi yoyote, juhudi hizo baadhi zinafanana na nyingine ni
tofauti kutokana na nchi na nchi, lakini sisi (Wachina) tulifahamu
kwamba tuna ardhi kubwa sana, hivyo tukaamua kuimua rasilimali hii kwa
kila namna iliyo bora. Licha ya eneo kuwa kubwa lakini tumehakikisha
hakuna eneo linaloachwa bila faida", alisema.
Kwa upande wake Kinana aliupongeza
uongozi wa China chini ya chama cha CPC na wananchi wa nchi hiyo kwa
kuweza kufanikisha kuinua uchumi wa nchi hiyo kwa kiwango kibwa cha
sasa.
"Bila shaka ni uchapakazi usio na
kikomo na wakujituma sana kwa pamoja kati ya serikali na wananchi ndiyo
maana mmefanikiwa hivi, napenda kuchua fursa hii niwapongeze kwa dhati
kwa mafanikio haya, nasi kama nchi rafiki tunapata kiu kubwa kuhakikisha
tunafika mlipo au angalau kuwakaribia", alisema Kinana.
Kinana yupo nchini China akiambatana
na ujumbe wa viongozi na maofisa wa Chama kwa ajili ya ziara ya mafunzo,
katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kisiasa, na pia kudumisha
urafiki wa kindugu wa siku nyingi kati ya Chama Cha Mapinduzi na Chama
Cha Kikomunisti cha nchi hiyo.
Katika ziara hiyo Kinana amefuatana na
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, Mjumbe wa Kamati
Kuu ya CCM, Khadija Aboud, Katibu wa NEC, Siasa na Uhuaisno wa
Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM,
Martine Shigela, Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi, Khamis Suleiman Dadi
na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi Mohammed Yusuf Mohamed.
Wengine ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Iringa, Jesca Msambatavangu, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Titus
Kamani, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na maofisa wa
Chama. ziara hiyo
Kinana anafanya ziara hiyo kutokana
na mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China, na anafanya ziara hiyo
ikiwa ni ya kwanza kuifanya nje ya nchi, tangu alipoteuliwa kuwa Katibu
Mkuu wa CCM, Oktoba mwaka jana mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment