MBATIA AJITOA TUME YA KUCHUNGUZA KUSHUKA KWA ELIMU
Na: Patricia Kimelemeta na Fidelis Butahe, Mwananchi
Mwenyekiti
wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amejitoa kwenye Tume ya
serikali kuchunguza chanzo cha kushuka kwa kiwango cha kutisha cha
matokeo ya kidato cha nne, iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Mbatia ambaye ametajwa kuwa mmoja wa wajumbe wa tume hiyo yenye wajumbe
15, alisema kamwe hatoweza kufanya kazi yake kwa uhuru kwa sababu ni
Mbunge wa kuteuliwa, kamati hiyo
imeundwa na serikali hivyo lazima kutakuwa na mgongano wa maslahi.
Hatua
hiyo imekuja siku tatu baada ya chama hicho kumwandikia barua Rais
Jakaya Kikwete, kikimuomba aunde tume ya kudumu ya elimu nchini.
Tume
hiyo iliundwa kutokana na matokeo mabaya ya mtihani wa kidato cha nne,
watahiniwa 240,903 kati ya 480,036 waliofanya mtihani walipata alama
sifuri, huku 23,520 sawa na asilimia 5.16 wakifaulu na wengine 103,327
sawa na asilimia 26.02 wakipata daraja la nne.
Januari
31, mwaka huu katika kikao cha bunge, Mbatia aliwasilisha hoja binafsi
kuhusu udhaifu katika sekta ya elimu akielezea kwa kina, sera ya elimu
iliyopitwa na wakati, kukosekana kwa mitalaa, kuwapo kwa mihtasari
mibovu ya masomo na vitabu kuwa na viwango duni.
Hata hivyo, wabunge wa CCM wakishirikiana na Serikali walimaliza hoja hiyo bila kutolewa majibu ya msingi.
Mbatia
alisema jana kuwa hawezi kufanya kazi yake kwa ufanisi ndani ya tume
hiyo, kwa sababu ndiye aliwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu udhaifu
sekta ya elimu, hoja ambayo ilizimwa bila kutolewa majibu ya msingi.
“Kamati
ya Waziri mkuu haina jipya la kufanya kwa sababu ipo Kamati iliyoundwa
mwaka 2011 kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne, imeeleza kila
kitu na ripoti ipo ofisi ya waziri mkuu, sasa hii ya sasa inakwenda
kuchunguza nini?” alihoji Mbatia.
No comments:
Post a Comment