TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Sunday, March 17, 2013

HII NDIO DALADALA AMBAYO DEREVA WAKE KAPIGWA RISASI AKIWA KWENYE FOLENI SINZA


Tukio lilitokea Ijumaa usiku kwenye saa tatu kasoro Sinza Kumekucha Dar es salaam karibu na kanisa la KKKT ambapo ilikua ghafla mlio wa risasi ukasikika ikiwa imelengwa kwa dereva wa daladala.
Watu waliokuwepo karibu wamesema dereva wa hii daladala anadaiwa kumkosea na kumkasirisha mtu wa pikipiki alipokua kwenye foleni.

Ghafla mtu huyo wa pikipiki ambae hakufahamika akiwa amebeba abiria inadaiwa alipita kwa mbele akachomoa bastola na kupiga risasi na kuondoka.

Inadaiwa dereva wa daladala aliepigwa risasi kichwani, alifariki muda mfupi baada ya tukio hilo huku watu wakishuhudia abiria mbalimbali wakitokea madirishani na wengine wakitoa vitu vyao kupitia madirishani.

mpekuzi inaendelea kufatilia hii taarifa ili kupata taarifa za uhakika kutoka kwa wahusika, wakiwemo polisi

No comments:

Post a Comment