RAIS WA CHINA KUFUNGUA JENGO LA UKUMBI WA MKUTANO LA KIMATAIFA
Hassan Silayo-Maelezo
Rais
wa ChinaXi Jinping anatarajia kufungua jengo la ukumbi wa mikutano wa
kimataifa la Julius Nyerere Convertion Centre lililopo jijini Dar -es
-Salaam linalomilikiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa wakati wa ziara yake nchini inayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa
wiki ijayo.
Hayo yamesemwa jana naKatibu Mkuu wa wizara hiyo John Haule wakati wa ziara ya kamati ya
Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walipotembelea jengo
hilo ili kuona maendeleo ya ujenzi.
Haule
alisema kuwa ujenzi wa ukumbi huo ni matunda ya mahusiano mazuri ya
ushirikiano yaliyopo baina ya Serikali ya China na ya Tanzania kwa
makubaliano maalum ikiwa kama msaada na mkopo nafuu usio na riba
ambao utalipwa kwa awamu mbili tofauti.
“Ukumbi
huu ni wa kisasa ,utatumika kama sekta ya utalii na biashara utasaidia
kuliingizia Taifa fedha za kigeni kwani una sehemu kubwa ya kuegesha
magari 222, chumba cha habari,mgahawa,ofisi za wazi na maktaba ndogo”,
alisema Haule.
Aidha
Haule alisema kuwa ziara ya Rais Xi Jinping ni kuimarisha mahusiano
baina ya Tanzania na China na kueneza sera ya mambo ya nje kwa kipindi
chote cha utawala wake atakachokuwa madarakani.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni mbunge wa Monduli
Edward lowassa alisisitiza umuhimu wa utunzanji wa jengo hilo na
kukamilisha mapema vitu ambavyo havijakamilika ili viweze kufanyiwa
kazi kabla ya ufunguzi.
Ujenzi
wa ukumbi huo wenye ghorofa tatu na kumbi nne za mikutano zenye uwezo
kupokea washiriki zaidi ya 1800 ulianza mwaka 2009 na umegharimu dola
za kimarekani milioni 29.7.
No comments:
Post a Comment