MWANA FA AITAKA SERIKALI IRUDISHE MFUMO WA ANALOJIA
Akiongea na gazeti la Habari Leo, FA amesema kwa sasa wasanii nchini
wanaumizwa na mfumo wa digitali kwakuwa wamekuwa wakitumia fedha nyingi
katika kutengeneza video, lakini zinaishia kutazamwa na watu wachache
tu wenye ving’amuzi.
“Waachie mifumo yote kwani kila mtu atakuwa na uamuzi wa kufanya, kutokana na ubora wa kazi,” alisema Mwana FA.
Alisisitiza kuwa huenda akasubiri hata miezi miwili na zaidi, kama serikali itakubali kuachia mifumo yote miwili wa digitali na analojia, na kama hawatotaka, basi ataachia hivyo hivyo kwa kuwa hawezi kukaa nayo ndani.

No comments:
Post a Comment