RIPOTI: MWENYEKITI WA SIMBA ,ndg, RAGE NA KAMATI YAKE YA UTENDAJI WANG'OLEWA
MKUTANO
mkuu wa dharura wa wanachama wa klabu ya Simba umemwondoa madarakani
mwenyekiti wao Ismail Rage na kuivunja kamati ya utendaji ya klabu hiyo
kwa madai ya kukiuka katiba ya klabu yao.
Mkutano
huo ambao kabla ya kufanyika kwake ulikuwa umepigwa marufuku na uongozi
wa Simba kwa madai kwamba haukuwa halali ulifanyika kwenye Hoteli ya
Starlight jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na
wanachama zaidi ya 600.
Mbali
ya kumtimua Rage,mkutano huo pia ulimpendekeza aliyekuwa mwenyekiti wa
kamati ya usajili Zacharia Hans Pope na Rahma AL kharoos kuongoza
kamati maalumu hadi pale uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utakapofanyika.
Mkutano
huo uliokuwa chini ya uenyekiti wa Mohamed Wandi na katibu wake Maulid
Said ulikuwa na agenda kuu moja iliyojadili mwendendo mbovu wa klabu
ya Simba kwenye Ligi Kuu inayoendelea na kutokuwa na imani viongozi.
Akizungumza
wakati akifungua mkutano huo uliokuwa na utulivu mkubwa huku ukilindwa
na askari polisi wachache,Wandi alimlaumu Rage kwa madai kwamba amekuwa
akiiendesha klabu yao pasipo kufuata katiba.
"Ibara
ya 16 kipengele G inasema kutakuwa na mkutano kila baada ya miezi
minne kujadili maendeleo ya klabu lakini haujafanyika mpaka leo.
"Vilevile
ibara ya 18 kipengele cha sita inasema kamati ya utendaji itaunda
baraza la wazee na kifungu cha 28 C,kutakuwa na nafasi ya mwanamke
katika kamati ya utendaji lakini imekiukwa,huku ni kusigina
katiba,".alisema Wandi na kuongeza kuwa:
"Ibara
ya 22 ya katiba ya klabu ya Simba itupanawapata wanachama haki ya
kuitisha mkutano endapo mwenyekiti na makamu mwenyekiti hawatakuwapo na
ibara ya 19 kifungu cha tatu inatupa mamlaka ya kumwandikisha na
kumfukuza mwanachama,".
Baada
ya kumaliza kusoma sehemu ya katiba ya klabu ya Simba aliyodai
imekiukwa,Wandi aliwataka wanachama wenzake kuamua kama Rage na kamati
yake ya utendaji ipewe muda zaidi au iondolewe ndipo wote waliponyoosha
mikono juu wakitaka watimuliwe.
No comments:
Post a Comment