KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS KUZINDULIWA LEO
Meneja
wa bia ya Kilimanjaro Bw. George Kavishe akizungumza na waandishi wa
habari katika ofisi za TBL Masaki wakati alipozungumzia uzinduzi wa Tuzo
za Kilimanjaro Music Award na kuasiniwa kawa mkataba wa udhamini wa
Tuzo hizo kati ya kampuni ya TBL na
BASATA.
Kushilla Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL akibadilishana hati na Godfrey Mngereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, huku viongozi wengi9ne wa TBL na BASATA wakipiga makofi.
Tuzo
za muziki maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013
zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam zikiwa na dhumuni kubwa la
kutambua wasaniii waliopata mafanikio katika sekta ya muziki kwa kipindi
cha mwaka mmoja uliopita.
George
Kavishe, Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager amesema
wakati wa uzinduzi huo kuwa, “Kilimanjaro Premium Lager inajivunia
kuendelea kudhamini tuzo hizi kwa mara ya 12 sasa lengo likiwa kukuza
muziki nchini Tanzania. Mchakato wa kuwapata wanamuziki bora wa mwaka
unaanza leo na utamalizika tarehe 8 Juni ambapo tutakuwa na hafla ya
usiku maalum wa kwa ajili ya kutangaza washindi.”
Alisema
Kilimanjaro Premium Lager imejizatiti kuendeleza tasnia ya muziki
Tanzania kwa kutambua na kuwapa tuzo wasanii wenye vipaji. ‘Tunataka
wanamuziki wetu wajisikie wanathaminiwa na kutambuliwa kwa kazi nzuri
wanayoifanya vile vile tunataka Watanzania waweze kuthamini muziki wa
nyumbani na kutambua mchango wa wanamuziki katika kuleta maendeleo ya
uchumi katika nchi.
‘’Kilimanjaro
Premium Lager inajivunia kuwa sehemu ya tuzo hizi na ni matumaini yetu
kua mwaka huu tukio hili litakua kubwa na zuri zaidi’’
‘’Pia
tuna furaha kutangaza kwamba BASATA imetupatia leseni ya kuendelea
kudhamini tuzo hizi kwa kipindi cha miaka mingine mitano. Kusainiwa kwa
mkataba mpya na BASATA ni uthibitisho wa azma kubwa tuliyonayo katika
kuendeleza muziki wa Tanzania. Mkataba huu utaifanya Kilimanjaro Premium
Lager kuwa mdhamini wa tuzo hizi mpaka mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment