MATOKEO YA UCHAGUZI KENYA: MFUMO WA ELEKRONIKI UMEKWAMA....ZOEZI LINAANZA UPYA
Huku Wakenya wakiendela kusubiri kwa hamu kubwa kumjua mshindi wa kura ya urais kufuatia uchaguzi wa Jumatatu, wasiwasi unaongezeka baada ya kukwama kwa mfumo wa uwasilishaji matokeo kwa njia ya elekroniki.
Kufuatia
hitilafu hiyo, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC) imesema
kwamba inategemea sasa matokeo yatakayowasilishwa na wasimamizi wa
uchaguzi kutoka majimbo yote 290 kote nchini ili kuanza upya shughuli ya
kujumlisha kura za urais.
“Maafisa
wetu wa usimamizi wa uchaguzi wanatarajiwa kuleta matokeo rasmi wakati
wowote kuanzia sasa. Tutaanza kutangaza matokeo rasmi kutoka maeneo
bunge yote 290 kuanzia hapo kesho”. Alisema Mwenyekiti wa IEBC, Isaack
Hassan, hapo jana jioni baada ya kukwama kwa mfumo wa kuwasilisha
matokeo kwa njia ya elektroniki.
Hassan
amedokeza kwamba idadi ya kura za urais zilizoharibika au kukataliwa
zitajumuishwa na kura zote zilizopigwa ili kupata hesabu ya asilimia ya
kura kwa kila mgombea.
Wafuasi wa muungano wa Jubilee.
“Kwa
mujibu wa katiba jaduali la matokeo litarekebishwa kuonyesha asilimia
ya kura kwa kila mgombea kuzingatia kura zilizopigwa.”
Ikiwa
hilo litafanyika, inamaanisha kwamba hakuna mgombea atakayepata
asilimia 50 ya kura zote na hivyo kupelekea kufanyika kwa duru ya pili
ya uchaguzi.
Hatua
hiyo imezua wasiwasi mkubwa kwenye muungano wa Jubilee ambao mgombea
wake, Uhuru Kenyatta, amekuwa akiongoza kwa asilimia 54 huku mpinzani
wake Raila Odinga wa muungano wa CORD akiwa na asilimia 42 kufikia jana
jioni.
“Sisi
muungano wa Jubilee tuna wasiwasi. Kwani hatujui ni nini kimesababisha
mabadiliko haya ya ghafla ya kukusanya matokeo na tunataka kuamini
kwamba hii sio njama ya kuunyima ushindi wa muungano wa Jubilee kama
inavyoonekana. Tunamtaka mwenyekiti wa tume uchaguzi atueleze." Alisema
mgombea mwenza wa muungano huo, William Rutto.
Baadhi
ya wagombea wamemiminika katika ukumbi wa Bomas kulalamikia kuchelewa
kuwasilishwa kwa matokeoya kura ya urais. Pia kumekuwa na visa kadhaa
vya udanganyifu vilivyoripotiwa kutoka vituo mbali mbali nchini.
Kinachosubiriwa
sasa ni maafisa wasimamizi wa uchaguzi kuja na fomu za matokeo ya kura
hiyo ili yajumuishwe kwa mkono na Tume iweze kutangaza rasmi matokeo ya
kura ya urais.
No comments:
Post a Comment