MANYARA WABEBA TAJI LA MISS TOURISM
Mshindi wa Tuzo la Vipaji akiwa anafuraha Muda Mchache baada ya kutangazwa kuwa yeye ndiye mshindi.
Hatimaye Mshiriki wa Miss Utalii
Tanzania 2012/13 kupitia mkoa wa Manyara wake imeshinda tuzo la vipaji
2012/13 na kuibwaga mikoa mengine wa mikoa 29 ya tanzania bara na
zanzibar Mary 19 alionesha vipaji vya hali ya juu katika ushindani ambao
ulikuwa mkubwa hasa kutoka kwa warembo wa mikoa ya Lindi , Kagera, Dodoma, Zanzibar, Katavi, hata hivyo
mchuano ulikuwa mkali zaidi kati ya
Miss Utalii, Lindi Manyara na Kagera ambao walionesha Umahili mkubwa wa
kucheza ngoma za asili na kupelekea kuingia katika hatua ya Tatu Bora.
Katika Hatua hiyo ya Tatu Bora washirika hao walicheza wimbo mmoja
ujulikanao kwa jina la katope kutoka kundi la ngoma za asili la kibiriti
ambao ni mchanganyiko wa ngoma mbalimbali wa makabila ya ngoma za
kusini.
Katika Hali iliyo wafanya wapenzi wa
Fani ya Urembo waliofulika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala kuto
kuamini kwamba wanao cheza jukwaani ni Mabinti wa Kizazi kipya ambao kwa
Hali ya kawaida ya sasa ni nadra sana kumuona sister Duu tena Mrembo
kucheza ngoma za asili kwa ufasaha na umahili mkubwa. hivyo kuwafanya
wapenzi hao kuacha viti vyao na kuanza kushangilia kwa nguvu mwanzo hadi
mwisho huku wakiwapongeza waandaaji wa shindano la Miss Utalii Tanzania
kuwa ni Hazina kubwa ya utamaduni wa Mtanzania na Wengine wakithubutu
kusema Miss Utalii ni mtambo wa kurekebisha tabia kwa kuweza
kuwabadirisha fikra za mabinti hao wa kizazi kupya mashindano hayo kwa
ya kuwa kucheza ngoma za asili ni ushamba hadi kuwafanya kuwa wacheza
ngoma mahili tena hadhalani bila ya Aibu na kwa kujivunia utamaduni na
Ngoma za Asili Tanzania. Wengi wa wapenzi waliohudhulia katika
shindano hilo wakisika kwa nyakati
tofauti kuitaka na kuishauli serikali na mamlaka za utalii kudhamini
shindano la Miss Utalii Tanzania kwa Faida ya Jamii na Taifa kwani
shindano hili limedhihilisha uwezo mkubwa wa sio tuuu kuhifadhi
utamaduni wa mtanzania bali pia kuhamasisha na kutangaza utalii wa
tanzania kitaifa na kimataifa.
Alisikika Mpenzi Mmoja aliye julikana
kwa jina La Jafary Shaibu akisema kuwa shindano hili ni zuri na ni
lakipekee lakini tatizo inaonekana waandaaji hawajapata wadhamini wa
uhakika, kwanini Serikali isiwasaidie hawa?
Akizungumza katika Shindano hilo
ambalo Mwanamuziki wa Kimataifa Che Mundugwao alikonga nyoyo za watu kwa
Muziki wake wenye asili ya kitanzania, Mgeni Rasmi Muheshimiwa Maabad
Suleiman Hoja Mustahiki Meya wa Manispaa ya Temeke aliwapongeza sana
washiriki na washindi lakini alitoa shukurani za pekee kwa waandaaji wa
mashindano haya kwa kuipa manispaa na wilaya ya Temeke Heshima kubwa ya
kuwa wenyeji wa Tukio hili la kitaifa lenye hadhi ya jimataifa
alisema kwamba hii ni heshima kubwa
kwa Manispaa ya Temeke wilaya ya Temeke Tunao uwezo na Hadhi kuwa
wenyeji wa matukio makubwa ya kimataifa na kitaifa kama hili la miss
utalii tanzania 2012/13. Hivyo kutoa fulsa ya pekee kwa Temeke
kujitangaza kitlii, kitamadunina kiuwekezaji ndani na nje ya Nchi,
aliahidi kuwa manispaa ya Yemeke inatawaunga mkono kwa Hali na Mali ili
kufanikisha fainali hizo ambazo zitafikia kilele katika ukumbi wa Dar
Live Mbagala Dar es salaam pia aliwataka wadau mbalimbai kujitokeza
kudhamini shindano hilo.
Mshindi wa Tuzo hiyo ya Vipaji ambaye
alishangiliwa na washiriki wote baada ya kutangazwa kama mshindi,
alizawadia Scholarship ya kusoma kozi ya Kiwango cha Diploma katika
chuo chochote nchini.
Fainali za Taifa za Miss Utalii
Tanzania mwaka huu Zimedhamiwa na: Mtwana Catering Services, Ikondolelo
Lodge, Zizou Fashion, Coca Cola Kwanza, VAM General Suppries
Limited,Global Publishers, TANAPA, Ngorongoro Crater, Lakeland Africa,
Clouds Media Group, Star Tv, Vailey Spring,Dotinata Decoration,Tone
Multimedia Group, Baraza la sanaa la Taifa (BASATA ) www.misstourismorganisation.blogspot.com
Muheshimiwa Meya wa Manispaa ya Temeke Maabadi Suleiman Hoja Akimvisha tuzo la vipaji Mshindi kutoka Mkoa wa Manyara.
Washiriki walio ingia tatu Bora wakiwa katika picha ya Pamoja na Mustaiki meya
No comments:
Post a Comment