TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Thursday, March 14, 2013

..

Walinzi wawili wa mke wa Rais wa Uganda Mama Museveni, walitolewa nje ya ukumbi wa bunge la nchi hiyo baada ya kuingia wakionekana wamebeba bastola ambazo waziwazi wengi waliziona.
Kilichofanya watolewe ni malalamiko ya Wabunge kadhaa akiwemo Joseph Sewungu ambae alieleza kuogopa baada ya kuziona hizo bastola huku wengine baadhi wakisema hawajioni kama wako salama.
Mbunge wa Mbale Jack Wamayi aliuliza kulikoni mpaka walinzi hao wa mama kuruhusiwa kuingia na bastola wakati walinzi wa baba ambae ndio Rais hawajawahi kufanya kitendo kama hicho.

No comments:

Post a Comment