WANAFUNZI 10,000 WALIOKATA RUFAA YA KUFELI MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012, WAMEFELI TENA
Wakati tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012 ikiendelea na kazi, imebainika kuwa wanafunzi waliokata rufaa kutaka mitihani yao isahihishwe upya wamefeli zaidi baada ya
kusahihishiwa.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Baraza la Mitihani
la Taifa (NECTA) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambazo
zimethibitishwa na baadhi ya maofisa, wanafunzi waliokata rufaa wamefeli
zaidi na hata walioongezewa alama matokeo hayakubadilisha madaraja
waliyopata awali.Habari zinaeleza kuwa, wanafunzi waliokata rufaa NECTA
kutaka mitihani yao isahihishwe upya ni takribani 10,000 na kwamba
baraza bado limetoa muda zaidi kwa wengine wanaotaka kukata rufaa.
Vyanzo
vya habari kutoka ndani ya NECTA viliieleza NIPASHE kuwa mitihani kwa
wanafunzi waliokata rufaa ilianza kusahihishwa Machi 12 na kuhitimishwa
Machi 15, mwaka huu na kwamba wengi wamefeli zaidi.“Baada ya wanafunzi
kadhaa kukata rufaa, NECTA iliamua kuwaita walimu waandamizi katika
masomo yote na kuanza kufanya kazi ya kusahihisha mitihani hiyo upya kwa
umakini, kilichowashangaza walimu hao ni kuona kiwango cha kufeli
kimeongezeka,” alisema ofisa mmoja wa NECTA ambaye aliomba jina lake
lisiandikwe gazetini kwa maelezo kuwa siyo msemaji wa baraza hilo.
Wakizungumza
na NIPASHE, baadhi ya walimu walisema walioshiriki kusahihisha mitihani
hiyo walisema kuwa maoni yaliyokuwa yanatolewa na baadhi ya watu kwamba
matokeo mabaya ya mtihani huo yalitokana na uchakachuaji, hayakuwa ya
kweli.Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Joyce Ndalichako, akizungumza na
NIPASHE jana alithibitisha kuwa mitihani ya wanafunzi waliokata rufaa
ilianza kusahihishwa Machi 12 mwaka huu.
Dk
Ndalichako alisema hata hivyo, hana taarifa kama matokeo ya wanafunzi
hao yanaonyesha kuwa wanafunzi wengi wamefeli zaidi kwa kuwa alikuwa
safarini kikazi.“Unavyozungumza na mimi nipo Arusha na wageni, sifahamu
kama baada ya kusahihishwa upya mtihani wa wanafunzi waliokata rufaa
matokeo yamekuwaje, nitafahamu baada ya kurejea Dar es Salaam Jumatano
wiki hii,” alisema Dk Ndalichako ambaye hata hivyo, hakutaja idadi ya
wanafunzi waliokata rufani.Dk Ndalichako alisema suala la kufeli zaidi
wanafunzi waliokata rufaa linawezekana kutokea kwa sababu kila mwaka
imekuwa ikijitokeza hali kama hiyo, hivyo ni jambo la kawaida
NIPASHE
No comments:
Post a Comment