TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Saturday, March 23, 2013

AY ANAKIPAJI CHA UIGIZAJI
 
Ambwene Yesaya ’AY’.
MSANII wa Bongo fleva ambaye alifanya vizuri katika filamu ya Girlfriend mwanzoni mwa miaka ya 2000, Ambwene Yesaya ’AY’ amefunguka kwamba yeye ni bonge la mwigizaji wa filamu na akiingia  moja kwa moja kwenye tasnia hiyo atawafunika wasanii kibao wanaoigiza hivi sasa.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, AY amesema kwa sasa ana mambo mengi yanayomfanya ashindwe kuigiza lakini kama kuna mwandaaji wa filamu akimuhitaji afanye muvi, basi ajipange na awe na mkwanja mrefu wa kumpa.
“Nilipanga kuandaa muvi na  (Hamis) Mwinjuma ‘MwanaFA’ lakini mambo yamekuwa mengi ila dhamira ipo palepale kama muda ukipatikana tutafanya muvi wadau wangu wakae mkao wa kula,” alisema.
Pamoja na hayo, Ay aliongeza kuwa kati ya wasanii anaowakubali katika tasnia hiyo ni Irene Uwoya kwani anafanya filamu kwa uhalisia.

No comments:

Post a Comment