Watu 40 wahofiwa kufukiwa baada ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Dar
Jengo lililoporomoka
Kuporomoka
kwa ghorofa hilo lililokuwa katika Mtaa wa Indira Gandhi, kulizua
huzuni, taharuki na simanzi kwa ndugu na jamaa waliofika kwenye eneo la
tukio kutaka kufahamu nini kimetokea.
Shughuli
mbalimbali katikati ya jiji hilo zilisimama kwa siku nzima baada ya
jengo hilo kuanguka na kusababisha vifo vya watu watano, 13 kuokolewa
huku zaidi ya watu 40 wakisadikiwa kufukiwa na kifusi cha udongo wa
jengo hilo.
Jengo
hilo lililokuwa likijengwa mkabala na Msikiti wa Shia Ithnasheri ulioko
Barabara ya Indira Gandhi na Kampuni ya ‘Lucky Construction Limited’
lilianguka majira ya saa 2.30 asubuhi wakati ujenzi ukiendelea juu huku
chini watoto wakicheza mpira na mama lishe wakiendelea na biashara zao
kama kawaida.
Pamoja
na vifo na wengine kujeruhiwa, magari takribani manne yalifunikwa na
kifusi cha jengo hilo na kupondwa pondwa na kuwa kama chapati.
Katibu
wa Msikiti wa huo wa Shia Ithnasheri, Mushtaq Damji alisema: “Leo
tulikuwa na kitu kama jumuiya kwa jamii ya wahindu, tulipanga
kusherehekea lakini yote yakafutika.
“Baada
ya swala ya alfajiri, watu walikuwa wanazungumza hapa na pale na baada
ya kupambazuka, watoto walikuwa wanacheza mpira, walikuwa 9. Sasa,
bahati nzuri watoto saba wakakimbia na watoto wawili wakawa wamekwama,”
alisema Damji.
Naye
Mlinzi wa Msikiti huo, Athuman Nassor alisema: “Mimi nafanya kazi ya
ulinzi hapa msikitini, lakini nilikuwa ninashangaa kiasi cha saruji
kilichokuwa kikitumika kukorogea zege, kweli walikuwa wanazidisha
mchanga.
“Niliwahi
kuwaambia hata hawa vibarua, kuwa hii inayofanyika mbona siyo…,”
alisema mlinzi huyo. Alisema; jana ilikuwa siku ya kumwaga zege ghorofa
ya 16 na kulikuwa na vibarua wapatao 50 ambao kila mmoja alikuwa na ndoo
yake tayari kuanza kazi kabla ya ghorofa hilo kuporomoka.
Mlinzi
huyo alisema kuwa wakati tukio hilo linatokea alikuwa mbali kidogo na
eneo la tukio na kusema kuwa bila shaka baadhi ya kinamama lishe ni
miongoni mwa waliofukiwa.
Endelea kusoma Gazeti la Mwananchi
Endelea kusoma Gazeti la Mwananchi
No comments:
Post a Comment