UPDATE ZA TUKIO ZIMA LA UPIGAJI KURA NCHINI KENYA
LEO wananchi wa Kenya wanapiga kura katika uchaguzi wao wa kihistoria wakiwa na katiba mpya. Zifuatazo na Updates kutoka BBC SWAHILI kuhusu tukio zima na upigaji kura:
16:27 Sehemu nyingi za starehe na
ulevi mjini Nyeri Mkoa wa Kati zimefungwa na zitafunguliwa Jumanne ili
kuwaruhusu wapiga kura kupiga kura.
Eneo la Mkoa wa Kati lina tatizo la
uraibu wa pombe.
16:24 Ng'endo Angela ambaye yuko
Mkoa wa Kati anasema kuwa kuwa sababu ya hitilafi za kimitambo, tume
imalzimika kutumia mfumo wa kawaida kwa kutumia daftari za wapiga kura.
Ni Nyeri peke yake ambako shughuli hiyo ilifanikiwa kwa njia ya
Elktroniki.
15:54 Mwandishi wa BBC Emmanuel
Igunza anasema kuwa foleni mjini Nakuru zimeanza kupungua na huenda
wapiga kura wakamaliza shughuli hiyo itimiapo saa kumi na moja jioni
muda wa mwisho wa kupiga kura.
15:16 Mmoja wa wagombea wakuu wa
urais Uhuru Kenyatta ameelezea masikitiko yake kuhusu yaliyojiri Mombasa
ambako washukiwa wa kundi la MRC waliwaua polisi na raia katika
mashambulizi usiku wa kuamkia leo. Lengo lao lilikuwa kuvuruga shughuli
ya uchaguzi.
14:57 Mwandishi wa BBC mjini
Kisumu, Ann Mawathe anasema milolongo ya watu imepungua sana katika
sehemu nyingi za mji huo ikizingatiwa kuwa asubuhi watu walikuwa
wamejaa.
14:51 Kuna taarifa kuwa magari ya
abiria yameanza kuongeza nauli ya magari kwa sababu ya upungufu wa
magari hayo wakati Wakenya wakiwa wamejitokeza kupiga kura.
13:33 Tume ya uchaguzi imeagiza
uachaguzi kurejelewa katika wodi tano kati ya zote 1'450 ambako mitambo
ya tume hiyo ilikumbwa na hitilafu pamoja na makosa kwenye karatasi za
kupigia kura.
13:31 Katika baadhi ya vituo vya
kupigia kura, ambako foleni ndefu zimeshuhudiwa, taarifa zinasema kuwa
watu wanaonekana kukata tamaa na wameamua kurejea nyumbani kwani foleni
hazisongi.
13:24 Mwandishi wa BBC Wanyama wa
Chebusire anaripoti kuwa gari la mbunge mmoja wa zamani limeteketezwa
moto katika kaunti ya Kakamega na watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa
mpinzani wake.
11:25 Mkuu wa Polisi David
Kimaiyo asema kuwa takriban wanachama 200 wa kundi la MRC au Mombasa
Republican Council walivamia kituo cha polisi wa doria wakiwa wanaelekea
kusambaratisha shughuli za kupiga kura. Inaarifiwa polisi wanne
waliuawa katika makabiliano kati yao na wanachama hao.
11:14 Mgombea wa urais Uhuru Kenyatta anapiga kura yake katika eneo bunge lake la Gatundu , mkoa wa Kati
10:39 Mwandishi wa BBC aliye mjiniNyeri Ng'endo Angela anasema kila baada ya nyumba kumi kuna kituo cha kupigia kura, wapiga kura wamejitokeza kwa wingi, baadhi ya mashine za tume ya uchaguzi zilifeli lakini baada ya kushughulikiwa mambo yakarejea kuwa sawa.
10:31 Mwandishi wa BBC mjini
Eldoret Wanyama wa Chebusire vituo vilifungua mapema mambo, yameenda
shwari kwa ujumla wake, lakini katika baadhi ya vituo, kumekuwa na
mushkil , mashine ziligoma katika kituo cha kupigia kura cha shule ya
msingi ya UG, zaidi ya wapiga kura elfu tatu , hadi sasa ni chini ya
watu hamsini wamepiga.
10:27 Mkuu wa tume huru ya
uchaguzi Isaac Hassan anahutubia waandishi wa habari kuhusu changamoto
inazokabiliwa nazo tyume hiyo. Isaac anasema vituo vilivyofungua
kuchelewa, vitahakikisha wapiga kura wote wamepiga kura.
10:22 Ingawaje tume ya uchaguzi
IEBC inawakubalia watu wawasindikize wazee au wagonjwa kupiga kura,
wapigaji kura wengine wanawakataza kufanya hivyo.
Mjini Kisumu katika
kituo cha upigaji kura cha Ukumbi wa Aga Khan, mwandishi wetu Ann
Mawathe dada mmoja alieyejipandikiza blanketi tumboni ili kuwahadaa watu
na akubaliwe kwenda hadi mwanzo wa foleni, alikatazwa kufanya hivyo na
wapiga kura wenzake.
Katika kituo hicho hicho, baba
fulani aliyekuwa amebeba kipochi cha mkewe aliyekuwa na mtoto mgongoni,
naye alirudishwa hadi nyuma kabisa ya foleni hiyo. Pia, mwanamume
mwingine aliyejitwika ufahari fulani kwa vile alikuwa kavalia suti, na
kutaka kuruka foleni, alikatazwa kufanya hivyo.
09:04 Waziri mkuu Raila Odinga
ambaye pia anagombea urais amepiga kura yake katika eneo la Kibera.
Amesema licha ya kupata habari za baadhi ya vituo vya kupigia kura kuwa
na hitilafu kidogo, wapiga kura wasiwe na wasiwasi kwani mambo yatakuwa
shwari.
08:43 Mgombea wa urais wa muungano wa CORD, waiziri mkuu Raila Odinga anatarajiwa kupiga kura yake wakati wowote kuanzia sasa.
08:30 Solomon Mugera anasema kwamba kupiga kura kunachukua takriban dakika 12.
08:25 Hassan Majid pia mwandishi
wa BBC anasema kuwa polisi wamepata mwili mmoja wa mtu aliyeuawa na
mwingine kujeruhiwa kwa kukatwa panga katika eneo la Mishomoroni.
08:24 Mwandishi wa BBC mjini
Mombasa, Karen Allen anasema kuwa polisi wamepata maiti za polisi wanne
ambao wameuawa katika eneo la eneo la Changamwe, Kaskazini mwa Mombasa.
Hana taarifa zaidi kwa sasa.
08:16 Frawaso Kimutai kupitia
Bofya facebook yuko katika kituo cha Menengai mjini Nakuru kura ilianza
kupigwa saa moja asubuhi na foleni ni ndefu ingawa inakwenda polepole
mwendo wa kobe.
08:15 Fatma Sanbur yuko mtaani
Kibera na anasema watu ni wengi sana lakini hakuna mbinu ya kupanga
foleni. Anasema watu wanapangwa kwa orodha ya majina na hata baada ya
saa moja tangu waanza kupangga foleni saa kumi na moja, shughuli ya
upigaji kura ilikuwa haijaanza.
07:52 Mombasa eneo la Kaloleni
mpiga kura mmoja amesema hadi kufikia sasa upigaji kura haujaanza kwani
maafisa wa tume ya uchaguzi bado hawajawasili na vifaa vyao.
07:50 Mwandishi wa BBC Ann
Mawathe yuko mjini Kisumu na anasema ameona foleni ndefu sana watu
wakiwa hamasa kupiga kura. Wamepiga foleni tangu saa nane usiku.
07:47 Eco Seyar Papa akiwa mjini
Nairobi anasema Wakenya wamejitokeza kwawingi jijini Nairobi katika eneo
la Dagoreti. Foleni zilianza kupigwa kuanzia saa tisa usiku tangu
kuanzishwa kwa demokirasia ncini Kenya watu waeneo hili hawajawai
kujitokeza kwa mapenzi kama inavyo onekana.
07:43 Upigaji kura bado haujaanza
katika baadhi ya sehemu za Kenya. Wapiga kura wanalalamika kuwa katika
vituo kadhaa tarakilishi zimegoma na kwa hivyo watasubiri muda kabla ya
kupiga kura zao.
07:32 William Ruto anasema kuwa
anajivunia uchaguzi wa Kenya unafanyika kwa amani licha ya dukuduku la
wengi. Anasema anawataka wapinzani kukubali matokeo ya uchaguzi vyovyote
matokeo hayo yatakavyokuwa.
07:28 Mgombea mwenza wa Uhuru Kenyatta, William Ruro amepiga kura mjini Eldoret.
07:24 Kips Oscar: Kupitia Bofya
Facebook yuko katika kaunti ya Marsabit anasema upigaji kura unaendelea
bila wasiwasi na kuwa wanatarajia shughuli itakamilika kwa muda bila
wasiwasi.
07:14 Hison Nyakundi : Yuko mjini Eldoret kwa Foleni tayari kupiga kura Bofya bbcswahili.
07:11 James Mwangi: Kwenye ukurasa wa Bofya Facebook wa Bofya bbcswahili anasema yuko kwenye foleni na habanduki.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment