TANZANIA YATAKA ISAIDIWE KUKUSANYA TAKWIMU
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu, Dr. Albina Chuwa ambaye anaongoza ujumbe wa Tanzania katika
Mkutano wa 44 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, Mkutano huo
unajadili taarifa mbalimbali zinazohusiana na masuala ya takwimu.
Tanzania ni Mjumbe wa Kamisheni hiyo. Akichangia majadiliano kuhusu
taarifa ya mpango wa uboreshaji na ukusanyaji wa takwimu za uhalifu,
Dr. Chuwa amesema, nchini
zinazoendelea Tanzania ikiwa moja wapo zinahitaji uwezeshwaji katika
eneo hilo hasa ikizingatiwa kwamba uhalifu baina ya nchi moja na
nyingine unatofautiana na kwa sababu hiyo hata ukusanyaji na uandaaji wa
taarifa na takwimu zake hauwezi kufanana kutoka na utofauti wa
kimazingira na uhalisia wa nchi husika na kusisitiza kwamba mpango
wowote kuhusu eneo hilo lazima uzingatie mahitaji ya nchi. Aliyekaa
nyuma ya Dr. Chuwa ni Mkurugenzi wa Shughuli za Takwimu, Bi.
Redegunda Maro.
Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi
(2012) Hajjat Amina Mrisho Said akifuatilia majadiliano kuhusu masuala
mbali mbali yahusuyo Takwimu katika Mkutano wa 44 wa Kamisheni ya
Takwimu ya Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Maalum
Tanzania imeshauri kwamba nchi zinazoendelea zisaidiwe katika ukusanyaji, uchambuzi na utayarishaji wa takwimu zinazohusu masuala ya uhalifu.
Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu,(NBS) Dr.Albina Chuwa, wakati alipokuwa akichangia taarifa kuhusu mpango Makati kuhusu wa uimarisha wa ubora na upatikanaji wa takwimu zinazohusu makosa ya jinai katika katika
ngazi ya Kitaifa na Kimataifa.
ngazi ya Kitaifa na Kimataifa.
Taarifa hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Takwimu na Geografia ya nchini Mexico kwa kushirikiana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Madawa na Uhalifu.
Dr. Chuwa anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa 44 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa.Mkutano huo unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ukiwakutanisha wataalam wa masuala ya Takwimu kutoka nchi mbalimbali.
Katika mchango wake, licha ya kuwashukuru waandaji wa taarifa hiyo, Mkuu huyo wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu amesema, ni vigumu kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania kuutekeleza
mpango huo kutokana na upana wake na vile vile kutozingatia uhalisia na mahitaji ya kila nchi.
mpango huo kutokana na upana wake na vile vile kutozingatia uhalisia na mahitaji ya kila nchi.
Dr.. Chuwa, kama ilivyo kuwa kwa wachangiaji wengine akabainisha kuwa hata aina ya makoja ya jinai yanatofautiana
kati ya nchi nchi na kwa sababu hiyo hata namna ya ukusanyaji wa taarifa zake unapashwa kuzingatia mahitaji ya kila nchi.
kati ya nchi nchi na kwa sababu hiyo hata namna ya ukusanyaji wa taarifa zake unapashwa kuzingatia mahitaji ya kila nchi.
“ Makosa ya jinai yanayotokea kwa mfano Tanzania hayawezi kulinganishwa au kufanana na yale yanayotokea nchini Marekani, kwa hiyo hata ukusanyaji wa taarifa zake, pia utatofautiana
kwa kuzingatia aina ya makoa ya jinai na mapana yake” akasisitiza na kuongeza.
kwa kuzingatia aina ya makoa ya jinai na mapana yake” akasisitiza na kuongeza.
Lakini “ jambo la msingi zaidi, ni kwamba kwa nchi kama Tanzania tuna hitaji kuwezeshwa ili ukusanyaji wa takwimu zinazohusu jinai, maandalizi yake na uainishaji wake uweze kuwa na ubora na viwango vya kimataifa.
Baadhi ya wajumbe wengine waliochangia ajenda hiyo, walikwenda mbali zaidi kwa kutaka
kuainishwa au kuwepo na tafsiri sahihi kuhusu jinai u, badala ya kuuweka makosa yote ya jinai katika kundi moja.
kuainishwa au kuwepo na tafsiri sahihi kuhusu jinai u, badala ya kuuweka makosa yote ya jinai katika kundi moja.
Aidha wajumbe wengine walitaka pia kuwapo kwa mafunzo, vipaumbele, uratibu na uwiano katika suala zima la ukusanyaji wa takwimu zinazohusu jinai .
Mkutano huo wa 44 wa Kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa, licha ya kujadili taarifa ya mpango mkakati wa kuimarisha ubora na upatikanaji wa takwimu za jinai , pia umejadili taarifa za takwimu nyingine nyingi zikiwamo zinazohusu masuala ya elimu, jinsia, mazingira, biashara, ajira, huduma, uchumi, viashiria vya maendeleo , sayansi na teknolojia, kilimo,sekta isiyo rasmi, takwimu zinazohusu bei, na takwimu zinazo husu afya.
No comments:
Post a Comment