WAWEKEZAJI WATAKIWA KUWEKEZA ARUSHA
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiwa anakata utepe wa lango la kuingia katika ukumbi wa World Garden uliozinduliwa leo jijini Arusha |
Na: Woinde Shizza ,Arusha
Mkuu
wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewataka wananchi wa mkoa wa Arusha
kuanza kuwekeza katika sekta mbalimbali ili kuweza kuweka mkoa huo
katika madhari na hadhi ya jiji. Aliyasema hayo jana wakati akifungua
jengo jipya la mikutano pamoja na ukumbi wa disco lililopo jijini hapa
lijulikanalo kwa jina la World garden lililopo katika kata ya
mshono ndani ya jiji la Arusha
Alisema
kuwa mkoa wa Arusha kwa sasa umepandishwa hadhi na kuwa jiji hivyo ni
wajibu wa wazawa kuwekeza katika mambo mbalimbali akitolea mfano kuwa
mpaka sasa pamoja ya kuwa wananchi ni wengi na wageni ni wengi lakini
mpaka sasa kuna sehemu super makerti moja tu kitu ambacho kinatia aibu
kwa jiji kubwa kama hili
Alisema
kuwa viwanja vipo vya kujengea sehemu hizo ni watu wa kuwekeza tu hivyo
aliwasihi wawekezaji wajitokeze kwa wingi kuwekeza katika vitu
mbalimbali ili kuweza kuwezesha jiji letu kuwa la kimataifa
Alibainisha
kuwa wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wanaogopa kwenda kuchukumikopo na
kuwekeza katika vitu mbalimbali lakini aliwatoa hofu na kuwaambia kuwa
mikopo ipo na ni haki ya kila mmoja kwenda kuchukuwa mkopo kwani nafasi
zipo wazi na mikopo ipo ya kutosha huku akibainisha kuwa amna
mfanyabishara yeyote mkubwa anafanya kitu pasipo kuchukuwa mkopo
Alipongeza
uongozi wa kampuni ya World Garden na kudai kuwa wameweza kupiga atua
kubwa kwani kufungua kwao kwa jengo hilo litasaidia kwa kiasi kikubwa
kwani vijana wengi watapata ajira kupitia jengo hilo kwani katika jengo
hilo kuna vitu vingi kwama vile ukumbi wa disco watu wa usafi wa nje na
mengine mengi ambapo watu wote wanaotakiw akufanya kazi huku ni
watanzania vijana hivyo watakuwa wamesaidia vijana kupata ajira
Kwa
upande wake mkurugenzi mtendaji wa World Garden alisema kuwa wao kama
kampuni yao inampango wa kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 120 na pia
alisema kuwa watajitaidi kuboresha vitu mbalimbali .
No comments:
Post a Comment