BABA MTAKATIFU AANZA WIKI YA KUFUNGA NA KUTOONEKANA HADHARANI
Baba
Mtakatifu Benedict wa 16 ameanza wiki yake ya mafungo ya kiroho ambapo
atakuwa haonekani hadharani kwa wiki nzima ikiwa ni mwanzo wa safari
yake ya kuelekea kuachia rasmi uongozi wa kanisa Katoliki na kusema kuwa
ana matumaini ibada zake zitakuwa na mafanikio.
Baba
mtakatatifu atabakia Vatican na baadhi ya wasaidizi wake wa karibu kwa
ajili ya ibada za awali za sikukuu ya Pasaka na atapata mapumziko mafupi
kila siku kwa ajili ya kuonana na katibu wake Georg Gaenswein, ili
kuyashughulikia masuala ya dharura ya kanisa.
Baada
ya wiki nzima ya ibada, Baba Mtakatifu atakutana na rais wa Italia,
Giorgio Napolitano, tarehe 23 Februari kushiriki ibada ya Jumapili yake
ya mwisho ifikapo tarehe 24 mwezi huu na kuzungumza hadharani kwa mara
ya mwisho mbele ya waumini wapatao 10,000.
Kiongozi
huyo wa kanisa Katoliki duniani ataachia uongozi rasmi tarehe 28 mwezi
huu na inasemakana kuwa Waziri wa Utamaduni wa Vatican Kadinali
Gianfranco Ravasi ndiye anayeonekana mtu mwenye nafasi kubwa ya kuchukua
nafasi yake kwa muda mfupi au mrefu.
No comments:
Post a Comment