TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, February 26, 2013

LADY JAYDEE NA PROF JAY NDANI YA NGOMA MOJA 

Profesa Jay na Lady Jaydee wanapokutana siku zote huwa hapaharibiki kitu, ni hit tu. Baada ya miaka mingi kupita, nguli hao wamekutana tena na guess what, this time hakuna amani kabisa kati yao, ni Joto na Hasira tu.

Unakumbuka Profesa Jay ameshawahi kumshirikisha Jide kwenye nyimbo zake mbili zilizohit sana enzi zake, Bongo Dar es Salaam na Nimeamini? Lakini kumbukumbu zetu hazituambii kama tulishawahi kusikia wimbo ambao Lady Jaydee amemshirikisha Profesa Jay. Hivyo huenda huu ndio ukawa wa kwanza.

Kupitia Facebook jana Lady Jaydee aliandika:

Naomba ku share muonekano wa ndani wa CD ya wimbo wangu mpya “JOTO, HASIRA” feat Prof Jay ambao unatoka siku za karibuni.” Lady Jaydee aliwaomba mashabiki wake wamsaidie kuchagua kava la wimbo huo.

No comments:

Post a Comment