TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, February 20, 2013

ASILIMIA ZA ALAMA ZA MATOKEO NI HAYA HAPA!

Kwa mujibu wa Jinsi matokeo  yalivyo, tunaweza kusema:
Kati ya wanafunzi 397,136 waliofanya mtihani; 240,750 walipata SIFURI!
- Division I - 1,641 => 0.41%
- Division II - 6,453 => 1.62%
- Division III - 15,426 => 3.88%
- Division IV - 103,327 => 26.02%
- Division 0 = [397,136 - (1,641+6,453+15,426+103,327)] -> 270,289 => 68.06%

  
---------------------------
Watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 wamepata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wanafunzi 103,327 sawa na asilimia 26.02 wamepata daraja la nne. 

Akitangaza matokeo hayo jana, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema watahiniwa walikuwa 456,137,

  • wa shule wakiwa 397,136 huku
  • wa kujitegemea wakiwa 68,806.
“Matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya sana, Serikali tunasikitika kutokana na hali hii lakini tuna mipango mbalimbali ya kuhakikisha tunaweza kutatua hili tatizo,” alisema Dk Kawambwa. 

Dk Kawambwa alisema watahiniwa wote kwa ujumla:

waliosajiliwa walikuwa 480,036 kati yao

  • wasichana 217,583 sawa na asilimia 45.3
  • wavulana 262,453 sawa na asilimia 54.67
​lakini waliofanya mtihani huo ni 456,137 sawa na asilimia 95.44, wengine 21,820 (asilimia 4.55) hawakufanya mtihani.
Alisema watahiniwa wa shule (school candidates) walikuwa 397,136 sawa na asilimia 96.57, miongoni mwao, 14,090 sawa na asilimia 3.43 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo utoro, ugonjwa na vifo.

Ufaulu kwa madaraja
Kwa mujibu wa matokeo hayo, watahiniwa waliopata

Daraja la kwanza ni 1,641,

  • wavulana wakiwa 1,073 na
  • wasichana 568,
Daraja la pili ni 6,453,
  • wavulana wakiwa 4,456 na
  • wasichana 1,997.
Waliopata daraja la tatu ni 15,426,
  • wavulana 10,813 na
  • wasichana 4,613, waliopata wa
Daraja la nne 103,327, 
 
  • wavulana 64,344 na
  • wasichana 38,983 huku
Daraja sifuri wakiwa 240,903,
  • wavulana 120,664 na
  • wasichana 120,239. 

No comments:

Post a Comment