
Eneo la tukio la ajali hiyo.


Kushoto
 ni gari ya Stive yenye namba za usajiri T 779 BZL na (kulia) ni gari 
lililohusika na ajali hiyo lenye namba za usajiri T 584 BQV.

Askari wa usalama barabarani, akipima ajali hiyo.

Askari akimkunja Stive na kumpakia katika gari lao ili kuondoka naye kumpeleka kituoni Mabatini.

Gari la Stive likiwa limebondeka kwa mbele lilikogongana na gari jingine.

Gari husika na ajali likiwa limetumbukia mtaroni.

Baadhi ya warembo walikuwa na Stive katika gari lake ambao ni miongoni mwa washiriki wa Movie hiyo, wakiwa eneo la tukio.
Movie
 mpya ya Msanii wa kuigiza sauti za Viongozi Stive Nyerere, iliyokuwa 
ianze kurekodiwa leo imeingia dosari baada ya msanii huyo kupata ajali 
na kuswekwa lupango katika kituo cha Polisi cha Mabatini, asubuhi hii.
Msanii
 huyo amepata ajali hiyo maeneo ya karibu kabisa na kituo cha Mabatini, 
wakati akiwa na msafara wa wasanii wenzake wanaoshiriki katika Movie 
hoyo, wakati wakielekea kuanza kurekodi.
Wasanii
 hao pamoja na Stive, walikuwa wakitokea katika Kambi yao iliyokuwa 
maalum kwa maandalizi ya kuanza kurekodi ikiwa ni pamoja na kufanyia 
mazoezi katika kambi hiyo iliyodumu kwa wiki kadhaa.
Ajali
 hiyo ilikuwa kama hivi:- Wakati Stive akiwa na baadhi ya washiriki wa 
movie yake katika gari lake na wakiwa katika mwendo kuelekea eneo la 
kushuti sini zao, ghafla aliona gari aina ya funcargo ikiwa imesimama 
mbele yake huku katikati ya barabara akiwapo jamaa aliyekuwa 
akisimamisha magari katika eneo hilo.
Baada ya kushindwa kusimama kwa ghafla ndipo alipoigonga gari hiyo kwa nyuma na gari hiyo kutumbukia mtaroni. 
Mashuhuda
 wa ajali hiyo walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni Fundi umeme 
aliyekuwa akisimamisha magari katika eneo hilo ili kuweza kuondoa waya 
wa Umeme uliokatika na kulala katikati ya barabara huku ukiwa na moto, 
ili kuepusha madhara zaidi.
Baada ya
 ajali hiyo, walifika askari Polisi wakiambatana na askari wa usalama 
barabarani, ambapo alianza kupima ajali hiyo huku madereva wakijibizana 
na fundi aliyesimamisha magari, ambapo majibizano hayo yaliingiliwa kati
 na mmoja kati ya askari waliofika eneo hilo.
Katika
 majibizano hayo baina ya fundi, Askari na madereva wote wawili, ndipo 
kulitokea kupishana kauli baina ya Stive na Askari huyo, aliyediriki 
kumuita Stive mjinga, ambapo Stive alishindwa kuvumilia na kuamua 
kumjibu na ndipo alipokunjwa 'Tanganyika Jeki' na kukokotwa hadi katika 
gari walilokuja nalo askari hao na kumpakia na kisha kuondoka naye 
kuelekea katika Kituo cha Mabatini. 
credits: Sufiani Mafoto

No comments:
Post a Comment