TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, February 12, 2013

WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WAPATIKANA





























Baadhi ya Wajumbe wa NEC ya CCM wameukwaa Ujumbe wa Kamati Kuu ya chama cha hicho katika kura zilizopigwa jana mjini Dodoma wakati wa kikao cha NEC kilichoongozwa na Mwenyekiti Rais Jakaya Kikwete.

Wajumbe kutoka Tanzania bara ambao hadi sasa majina yao yametajwa kushinda uchaguzi huo ni pamoja na Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Gongo la Mboto, Jerry Slaa, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi, Prof. Anne Tibaijuka , Mbunge Pindi Chana, aliyewahi kuwa Meya wa jiji la Dar es Salaam, Adam Kimbisa, Dk Emmanuel Nchimbi na Waziri William Lukuvi.

Waliochaguliwa kutoka Tanzania Visiwani (Zanzibar) ni pamoja na  Dk. Salim Ahmed Salim, Shamsi Vuai Nahodha, Profesa Makame Mbarawa, Dk. Hussein Mwinyi, Samia Suluhu Hassan, Dk Maua Abeid Daftari na Khadija Aboud.

Wajumbe hao 14 ni kati ya 28 ambao walipigiwa kura jana kuwania nafasi hiyo ya Juu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi.

No comments:

Post a Comment