PAPA WAWILI KATIKA MGONGANO

Na  VATICAN City, Vatican 
Kwa siku mbili, Papa amekuwa na 
shughuli nyingi katika makao yake, Gandolfo Castel, Vatican akijiandaa 
kimwili kuondoka, akiweka sawa nyaraka zake binafsi na zile za kanisa 
ambazo zitawekwa katika kumbukumbu.
 Kwa upande mwingine Vatican, nchi 
ambayo ipo ndani ya Jiji la Rome iliyozungukwa na ukuta, ikiwa na ukubwa
 wa hekta 44 na wakazi 832 pekee, imekuwa katika hekaheka nyingi.
Jana, waumini zaidi ya 50,000 na wengine wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wakiwamo makardinali, maaskofu, mapadri na walei walialikwa kwa shughuli rasmi ya kumuaga kiongozi huyo.
Jana, waumini zaidi ya 50,000 na wengine wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wakiwamo makardinali, maaskofu, mapadri na walei walialikwa kwa shughuli rasmi ya kumuaga kiongozi huyo.
Tofauti na kanuni yake, leo 
Benedict hatavaa viatu vyekundu kama ilivyozoeleka na badala yake 
amechagua viatu rahisi vya ngozi vilivyobuniwa Mexico. Alipewa viatu 
hivyo ikiwa ni zawadi wakati wa ziara nchini humo 2012.
Tangu alipotangaza uamuzi wake wa 
kung’atuka Februari 11, mwaka huu, utata umegubika nafasi yake katika 
maisha mapya ndani ya Vatican, akiitwa Papa Mstaafu.
Waumini, wataalamu na hata 
viongozi mbalimbali wa Kikatoliki wameanza kuhoji ni jinsi gani viongozi
 wawili (Papa) wataishi, huku wote wakivaa mavazi meupe wakiitwa Papa, 
wakiishi umbali mdogo kati yao, wakiwa na wasaidizi wengi 
wanaowahudumia.
Vatican
Nje ya Gandolfo Castel, ulinzi umeimarishwa na vibali vya kuingia Vatican vimesitishwa.
Juzi, Vatican ilitangaza kwamba Papa Benedict XVI atajulikana kama ‘Emeritus Pope’, yaani Papa Mstaafu mwenye cheo cha heshima, akiendelea kuitwa, ‘mtakatifu’ na ambaye ataendelea kuvaa nguo nyeupe.

Mavazi na hata jina lake jipya ni 
masuala ambayo yamezua uvumi mwingi, huku suala la mrithi wake mpya pia 
likiwa gumzo, kwani tukio kama hilo lilitokea miaka 600 iliyopita.
Ni uamuzi uliolishtua kanisa hilo lenye waumini 1.2 bilioni duniani na wengi wanasema awali, haikushauriwa Papa kustaafu kwani kwa kufanya hivyo kunaacha mizozo na minong’ono ya kuwania madaraka.
Ni uamuzi uliolishtua kanisa hilo lenye waumini 1.2 bilioni duniani na wengi wanasema awali, haikushauriwa Papa kustaafu kwani kwa kufanya hivyo kunaacha mizozo na minong’ono ya kuwania madaraka.
Hata hivyo, uongozi wa Vatican 
umesisitiza kuwa uamuzi huo wa Papa Benedict XVI ni wa kipekee na hakuna
 mzozo ambao utatokea baina yake na mrithi wake ambaye mchakato wa 
kumpata unatarajiwa kuanza ndani ya wiki mbili zijazo.
“Kulingana na mabadiliko katika 
kanisa letu, kuna Papa mmoja. Ni dhahiri kwamba katika hali ya sasa 
hakutakuwa na tatizo,” anasema Mhariri wa Gazeti la L’Oservatore Romano 
linalomilikiwa na Vatican, Giovanni Maria Vian.
Hofu iliyopo
Hata hivyo, wakosoaji wa mambo hawakubaliani na hoja hiyo na baadhi ya makardinali walioko Vatican kwa usiri mwingi, wanazungumzia suala hilo wakieleza kwamba litazua tatizo kubwa kwa Papa ajaye, hasa ikiwa mtangulizi wake, Benedict akiwa bado hai.

Mtaalamu wa tauhidi (theolojia), 
raia wa Uswisi, Hans Kueng ambaye amekuwa mtu wa karibu wa Papa Benedict
 XVI, ingawa kwa sasa ni mkosoaji wake amesema:
“Kwa sasa, Benedict XVI akiwa bado hai, kuna hatari ya kuwa na Papa kivuli, mwenye mamlaka kamili ambaye kwa chinichini anaweza kumshinikiza mrithi wake kufikia uamuzi.”
Hans Kueng alisema hayo alipozungumza na Gazeti la Der Spiegel la Ujerumani.

Msemaji wa Vatican, Padri Federico
 Lombardi alisema Papa Benedict XVI kwa upande wake aliamua aitwe Papa 
Mstaafu au ‘kiongozi mstaafu wa Roma.’ Anasema haelewi ni kwa nini 
ameamua kuacha jina lake la sasa la Askofu wa Rome.
Kwa wiki mbili zilizopita, maofisa
 mbalimbali wa Vatican wamekuwa wakifikiri kwamba Papa angeanza kuvaa 
mavazi meusi na kutumia jina la Askofu Mstaafu wa Rome ili kuepuka 
mkanganyiko na mrithi wake.
Mwingine ambaye amekuwa akizusha 
mkanganyiko ni Katibu wa Papa, Askofu Mkuu, George Gaenswein ambaye 
ataendelea kuwatumikia Papa wote wawili, yaani Benedict XVI kwenye 
Monasteri ndani ya Vatican na kazi yake ya kawaida ya kuwa kiranja 
katika nyumba ya Papa mpya.
Kwa upande wake, Papa Benedict XVI
 anasema anastaafu na sasa ataishi maisha ya sala na tafakuri ya kina, 
mbali na majukumu mengine ya kidunia.
Hata hivyo, bado atakuwapo kwenye nchi ndogo ya Vatican, mahali ambako makazi yake yatakuwa jirani na mnara wa kurushia matangazo wa Kituo cha Redio cha Vatican, akiliangalia vizuri Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Kwa upande wake, Kueng anasema ni 
kosa kwa Askofu Gaenswein kuwatumikia Papa wawili kwa wakati mmoja na 
pia Benedict XVI kubakia jirani na mahali hapo.
“Hakuna padri ambaye anapenda mtangulizi wake kuishi karibu naye na kufuatilia anayoyafanya.
“Hakuna padri ambaye anapenda mtangulizi wake kuishi karibu naye na kufuatilia anayoyafanya.
Hata kama Askofu wa Rome, haipendezi kutenda kazi huku mtangulizi wako akiona na kufuatilia.”
Mbali na mitazamo hiyo, wengine wamedhani kuwa uamuzi wa Papa Benedict XVI unalenga kudumisha utamaduni wa watangulizi wake.
Mbali na mitazamo hiyo, wengine wamedhani kuwa uamuzi wa Papa Benedict XVI unalenga kudumisha utamaduni wa watangulizi wake.
“Ninashangazwa kuona Papa Benedict
 XVI akiendelea kuitwa mbarikiwa na kuvaa nguo nyeupe,” anasema Padri 
James Martin, Mtawa wa Jesuit pia mwandishi na mhariri, lakini baadaye 
anajirudi na kusema:
“Lakini sioni ajabu, mbona marais wastaafu wa Marekani, bado wanaitwa Rais? ni alama ya heshima kwake.”
“Lakini sioni ajabu, mbona marais wastaafu wa Marekani, bado wanaitwa Rais? ni alama ya heshima kwake.”
Katika mkanganyiko huo, wapo 
wanaoamini kwamba yanayotokea yanatokana na nguvu ya roho mtakatifu, 
huku wengine wakipiga upatu kwamba ni zamu ya Afrika kutoa Papa na 
wanatajwa Makardinali Peter Turkson wa Ghana na Francis Arinze wa 
Nigeria.
No comments:
Post a Comment