TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Monday, February 18, 2013

MKONO WA MWANAMKE ALBINO ULIOKATWA SUMBAWANGA APATIKANA

























Juzi, vyombo vya habari viliripoti kuhusu, “Mwanamke albino anyofolewa mkono”.Taarifa mpya zilizopatikana kama zinavyoonekana pichani juu, ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya (wa tatu kulia) akibubujikwa na machozi jana usiku hali akushuhudia Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, Peter Ngusa (kulia) akiwa ameushikilia mkono ulionyofolewa hivi karibuni kutoka kwa mwanamke mwenye ulemavu wa ngozi (hayupo pichani) na kufukiwa porini kijijini Miangalua wilayani Sumbawanga.
Pichani juu ni Madaktari wa hospitali ya Mkoa Rukwa juzi, wakijaribu kumwekea damu bi Maria Chambanenje (39) aliyevamiwa na kukatwa mkono na watu wasiofahamika, huku wakichukua mkono wake.
Mama huyo ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) alikatwa mkono na watu wasiofahamika baada ya mumewe kwenda kulala kwa mke mwingine. Usiku watu wasiojulikana kuingia katika nyumba hiyo na kumkata mkono na kuondoka nao.

Kwa mujibu ya wakazi wa eneo hilo, mauaji kwa imani za kishirikina yanarejea kwa kasi.

No comments:

Post a Comment