TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, February 20, 2013

LULU AJIPANGA KUJIENDELEZA KIMASOMO
BAADA ya kupata dhamana msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ajipanga kujiendeleza na masomo ili aweza kupambana na changamoto za maisha.
Akizungumza na Maisha msanii wa filamu ambaye pia amekuwa ni mtu wa karibu  familia ya Lulu Mahfudh Hussein 'Dkt. Cheni' amebainisha kuwa Lulu yupo kwenye mchakato wa kurudi shule ili aweze kuendelea na masomo yake
Alisema kuwa ingawa familia ina mikakati hiyo suala kubwa linalokwamisha kwa sasa ni kipato kwani familia yake haina uwezo wa kumlipia msanii huyo na badala yake anatakiwa Lulu kuanza kufanya kazi ili aweze kujikwamua kwa hilo
Dkt. Cheni aliweka wazi kuwa kutokana na kipato cha familia ya msanii huyo hivyo anatakiwa kwa sasa aweze kufanya kazi ya filamu ili aweze kujimudu kama ilivyokuwa mwanzo na maisha yaendele
"Hapo awali alikuwa na uwezo wa kuihudumia familia yake kwa njia ya kazi zake alikuwa anamsomesha mdogo wake wa mwisho pamoja na kulipa kodi ya nyumba alikuwa akifanya mammbo mengi hivyo na swala la kusoma lijukumu lake pia" alisema
Mbali na hayo msanii Cheni alieleza kuwa Lulu yupo tayari kurudi shule ili aweze kujikwamua kielimu aweze kupambana na maisha hivyo jambo la msingi ni yeye kufikisha malengo yake aliyojipangia kwani umri wake bado ni mdogo na ananafasi kubwa ya kubadilisha maisha yake
Akizungumzia kwa upande wa kazi Dkt. Cheni aliweka wazi kuwa endapo Lulu akimuomba amsimamie kazi zake atafanya hivyo kwani yote ni katika nia njema ya kumfikisha msanii huyo katika malengo aliyojipangia

No comments:

Post a Comment