TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Tuesday, February 26, 2013

NMB WAPATA TUZO YA SUPER BAND

Mkuu wa masoko na mawasiliano wa NMB Imani Kajula akipokea tuzo ya super brand kutoka kwa mkurugenzi wa super brand East Africa Jawad Jaffer. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Mark Wiessing akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Clouds Media Group, Joseph Kussaga (Kulia) na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa NMB Imani Kajula. 
Baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa NMB wakiwa na tuzo ya super brand 2013-2014.

Tuzo ya Super Brand huwa inatolewa kwa kila kampuni ambayo jasho lake limeonekana, jitihada za ufanyaji kazi pamoja na kutimiza vizuri hata wakati mwingine kuvuka mipaka kwa yaliyoahidiwa.
Sasa baada ya miaka saba ya uwekezaji endelevu katika kuboresha huduma, masoko na mtandao wa matawi, benki ya NMB yenye zaidi ya matawi 148, ATM zaidi ya 500, wateja wanaotumia NMB mobile zaidi ya 800,000 na huduma mbadala  kama internet banking, kituo cha huduma kwa wateja na POS imepewa heshima na zawadi ya tuzo hiyo mwaka huu.
Jingine ambalo ni moja ya sifa kubwa zilizoipa heshima NMB ni kwamba wateja wake sasa wanapata huduma popote walipo bila kuhitajika kwenda kwenye tawi la NMB, maboresho hayo yameiwezesha NMB kutunukiwa kuwa Super Brand mwaka 2013-2014.

No comments:

Post a Comment