MWANA FA ADAI KUWA SIRI YA MAFANIKIO YAKE NI MATUMIZI MAZURI YA VIPAJI ALIVYO NAVYO
MSANII
 wa muziki wa kizazi kipya Hamis Mwinjuma 'Mwana Fa' aeleza, kuwa na 
kipaji zaidi ya kimoja ndio sababu ya kipekee inayomtofautisha yeye 
pamoja na kazi zake na baadhi ya wasanii wengine wa muziki wa bongofleva
Aliyazungumza
 hayo jijini Dar es Salaam wakati akielezea mikakati yake aliyokuwa nayo
 ya kuiachia nyimbo yake mpya hivi karibuni inayoitwa 'Kama 
Zamani'ambapo mashabiki wake watapata fursa ya kuisikia nyimbo hiyo 
katika vituo vya redio mbalimbali nchini, alisema kipaji ndicho 
kinachompa fursa ya kufanya muziki katika ngazi ya kimataifa
Alisema muziki unamatawi mbalimbali kwani kuna baadhi ya wasanii wanakipaji cha kuimba tu lakini hawezi kufanya shoo katika 'stage' wapo baadhi wanajua kuandika na hawajui kuimba wapo wengine wanajua kufanya vyote kwa wakati mmoja
Akizungumzia kwa upande wake Mwana Fa alisema amejaaliwa kuwa na vipaji vyote kwa wakati mmoja huku akiwa na uwezo wa kuandika mashairi, kuimba pamoja na kulimiliki jukwaa pindi awapo katika shoo
"Nimejaliwa vipaji vyote hivyo, kwani nina uwezo wa kuandika mistari mizuri, kuimba na kulimiliki jukwaa na ndio maana shoo zangu zinakuwa na mvuto wa kipekee kutokana, sanaa na ubunifu niliokuwa nao " alisema Mwana Fa
Akizungumzia ujio wa wimbo wa 'Kama zamani' wenye mahadhi ya Hip Hop ambapo msanii huyo amewashirikisha baadhi ya wasanii kama Man'dojo, Domokaya na The Kilimanjaro Band (Wana Njenje), alisema kuwa ameamua kushirikisha wasanii hao ili kuleta radha tofauti ya muziki na mashabiki wapate muziki ulio bora
No comments:
Post a Comment