RAY: MAZOEZI YAMENISAIDIA KUPUNGUA
Picha hiyo ya juu inamuonesha alivyokuwa mwanzo (kushoto) na jinsi alivyo sasa (kulia).
------------
------------
Muigizaji
 aliyepo kwenye list A ya waigizaji wa filamu Tanzania, Vincent Kigosi 
aka Ray ameamua kuzungumza baada ya watu kuanza kumzushia anaumwa 
kutokana na kupungua mwili wake kwa kiasi kikubwa.
Ray amezikanusha tetesi hizo zilizoanza kusambaa kwa haraka ambapo gazeti la udaku la Kiu wiki hii lilikuwa na habari isemayo, ‘Ray apukutika mwili’ – Kitambi chote kwishnei! Ukimuona unaweza kumpita bila kumtambua, maombi ya wakatoliki yahusishwa.
Hata hivyo Ray amesema hali hiyo imetokana na kufanya mazoezi zaidi siku za hivi karibuni. “Jamani kwani unene ndio afya au kupungua ndio ugonjwa,” ameuliza Ray.

No comments:
Post a Comment