MWAIKIBAKI ATEMBELEA KIWANDA CHA MAGEREZA
Rais wa
Kenya, Mwai Kibaki (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Magareza
nchini, Kamishna Jenerali John Minja kabla ya kuingia ndani ya Kiwanda
cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, anayefuata ni
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.
Rais wa
Kenya, Mwai Kibaki (wapili kutoka kulia) akiwa na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili kutoka kushoto), Mkuu wa
Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia) pamoja na maofisa
mbalimbali kutoka nchini na Kenya, wakiingia ndani ya kiwanda hicho.
Mshauri
Mtaalamu wa Mradi wa Kiwanda cha kutengeneza kofia ngumu katika Jeshi la
Magereza, Alpherio Moris (kulia) akimuonyesha Rais Mwai Kibaki moja ya
kofia ngumu (Helmet) ambayo inatarajiwa kutengenezwa na kiwanda cha
magereza Ukonga hivi karibuni.
Mkuu wa Jeshi la Magereza, Kamishna Jeneral John Minja (kushoto) akimkabidhi zawadi maalum ya kiti Rais Mwai Kibaki wa Kenya.
Rais Mwai
Kibaki (wa kwanza kutoka kulia aliyevaa tai) akiwafurahia Askari
Magereza na ofisa kutoka nchini Kenya wakiwa wamekaa kwenye kiti cha
wapendanao kilichotengenezwa na wafungwa kiwandani humo.
Rais Mwai
Kibaki (wa pili kushoto) akiwa na maofisa mbalimbali wakiondoka Kiwanda
cha Magereza Ukonga baada ya kumaliza kuangalia vifaa mbalimbali
vinavyotengenezwa na kiwanda hicho.
Rais Mwai Kibaki akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali nchini pamoja na maofisa kutoka nchini Kenya.
PICHA ZOTE NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment