Mtandao wa TMZ umeripoti kwamba
 rapper Drake alizuiwa kuingia kwenye club moja ya usiku huko Hollywood 
Marekani weekend iliyopita.
Sababu hasa ni kwamba hasimu 
wake, staa mwenzake ambae mwaka jana walirushiana chupa kwenye club moja
 ya usiku, mwimbaji Chris Brown tayari alikua ameshaingia ndani kwenye 
club hiyo hivyo mabaunsa walifanya kile walichoelekezwa cha kutoruhusu 
hizo sura mbili kuingia kwenye club hiyo kwa wakati mmoja.
Club nyingi sasa hivi zinahofia
 kuwaruhusu wawili hao kuwepo sehemu moja ili kuepuka yaliyotokea kwenye
 club waliyorushiana chupa ambayo ilifungwa kwa muda, pamoja na watu 
mbalimbali kudai fidia za kuumizwa kwenye ugomvi wa mastaa hao wawili 
ambao inaaminika ulikua ni wa kumgombania Rihanna.


No comments:
Post a Comment