NEEC NA NDC WASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO WA KUWAWEZESHA KIUCHUMI
Dk Anacleti Kashuliza Katibu
Mtendaji wa Baraza la Taifa La Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NCC
akibadilishana mikataba wa ushirikiano kuwawezesha wananchi na Kaimu
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa NDC Bw. Shannel
Mvungi
Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na Shirika la Taifa la
Maendeleo (NDC) wameanzisha ushirikiano utakaowawezesha wananchi
kiuchumi katika maeneo ambayo NDC imeanzisha miradi mbalimbali ya
maendeleo. Manufaa haya kwa wananchi yanatokana na kusainiwa kwa
Makubaliano ya ushirikiano kati ya mashirika haya ambao unalenga kutoa
fursa kubwa za ushiriki wa kiuchumi kwa wananchi wa maeneo husika.Hadi
sasa,
miradi inayolengwa ambayo inasimamiwa na NDC ni uchimbaji wa Makaa ya
Mawe ya Mchuchuma na Chuma cha Liganga Wilayani Ludewa unaotekelezwa
chini ya Kampuni ya ubia ya Tanzania China International Minerals
Resources Limited ambao unatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja zaidi
ya 5000 kwa watanzania ambazo ni fursa kubwa ya kukuza mapato ya
wananchi wa Ludewa.
Matarajio
ya NEEC na NDC ni kuwaendeleza na kuwawezesha kiuchumi wananchi walioko
katika maeneo ambayo miradi imeanza kutekelezwa ili waweze kujipanga
na kujiandaa vema kufaidika na fursa hizo kwa kufanya yafuatayo:-
- Kutoa mafunzo ya ujengaji uwezo na ujuzi katika kutambua fursa zilizopo na jinsi ya kuzitumia,
- Kuhamasisha fursa na miundo mbinu ya kiuchumi,
- Kuhamasisha kujiunga katika Mitandao ya Vikundi na Masoko,
- Uwezeshwaji wa Upatikanaji wa Mitaji na kuunganishwa na Taasisi za Fedha,
- Kuainisha na Kuendeleza maeneo huru ya Kufanyia Biashara na
- Kuhamasisha Umuhimu wa Ushirika
Lengo
la makubaliano ya ushirikiano huu ni kuweka mifumo ya utekelezaji na
usimamizi wa kuwaendeleza na kawawezesha wananchi katika maeneo ya
miradi mbali mbali inayosimamiwa na Shirika la Taifa la Maendeleo ili
waweze kunufaika vema na rasimali asilia zinazowazunguka.
Taasisi
hizi mbili zinatarajia kushirikiana vema katika kuwaunganisha wadau
mbali mbali wa maendeleo katika maeneo husika hususani wawekezaji wa
sekta binafsi,mashirika yasiyo ya kiserikali,wadau wa maendeleo na
serikali za mikoa na wilaya katika kuwaendeleza na kuwawezesha wananchi
katika maeneo husika.
Ni
matarajio ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) na
Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kuona rasilimali asilia
zikiwanufaisha wananchi katika maeneo yao kwa kuwawezesha kushiriki kwa
kiasi kikubwa katika shughuli za kiuchumi na kubadili hali zao za maisha
kupitia ongezeko la kipato na kuboreka kwa miundombinu.
Baraza
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) lilianzishwa chini ya
kifungu cha nne (4) cha Sheria ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi .
Baraza lilianza kazi rasmi mwaka 2005 likiwa ni chombo cha juu cha
kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.
Shirika
la Taifa la Maendeleo (NDC) ni chombo cha umma kinachomilikiwa asilimia
100 na Serikali, Shirika hilo lililoanzishwa mwaka 1965 kuchochea
maendeleo ya nchi kupitia viwanda katika sekta zote za uchumi.
No comments:
Post a Comment