NIKKI MBISHI AMMWAGIA SIFA KIBAO LADY JAY DEE
Nikki
 Mbishi ni rapper usiyeweza kumfananisha na yeyote Tanzania kwa uwezo 
wake usioelezeka katika uandishi wa haraka wa mashairi yenye mistari 
konde na uwezo wa kufanya mitindo huru (freestyle). Pia ana kumbumbuku 
ya ajabu na akiwa na uwezo wa kuimba nyimbo za wakongwe kama Profesa Jay
 na hata wa Marekani utadhani kaziandika yeye.

 Lakini
 pamoja  na maisha yake ya muziki kuzungukwa zaidi na utamaduni wa Hip 
Hop, Nikki aka Terabyte huchukua muda pia kusikiliza muziki laini wa 
wasanii wenzake wa Bongo na kwa mtazamo wake Lady Jaydee ndiye msanii wa
 kike anayemkubali kuliko yeyote.
“Leo nimeamka na dada mkuu tu @JideJaydee hakuna kama huyu kwenye historia ya wanamuziki wa kike Bongo @GraceMatata fuata huyo dada.,” ametweet Nikki Mbishi.
Rapper huyo controversial ameendelea kutweet majina ya nyimbo kibao za nguli huyo wa muziki wa Tanzania ambaye jina lake halisi ni Judith Mbibo.

No comments:
Post a Comment