JATA WAKABIDHI ZAWADI WANAFUNZI WALIOSHINDA INSHA ZENYE THAMANI YA DOLA ZA KIMAREKANI 800
Wanafunzi wakisikiliza kwa makini |
Faiza akionyesha zawadi yake ya LapTop aina ya HP aliyokabidhiwa baada ya kushinda kuandika Isha kwa alama alizopata ni 81 |
Faiza na mwalimu wake akimsindikiza kupokea zawadi |
Na Mwandishi wetu
SHIRIKA lilisilo la kiserikali toka Nchini Japan JICA ALUMNI ASSOCIATION OF TANZANIA (JATA) limetumia kiasi cha Dola 800 za
Kimarekani kutoa zawadi kwa wanafunzi wa
shule za sekondali nchini walioweza kuandika
na kuisoma insha iliyoandaliwa
na shirika hilo.
Mada ya isha hiyo ilikuwa inahusu Athari za Utandawazi wa kisasa kwa vijana wa Tanzania ,ambapo
jumla ya wanafunzi 31 walishiriki katika
shule sita zilizotoka Bara na Visiwani.
Katibu wa Shirika hilo Bi. Edina Ngerageza alizitaja shule zilizoshiriki kuwa ni Sunni Madressa , Kibaha , Wama
Nakayama,Zahanaki , Abbey, Kibamba.
Bi. Ngerageza alisema lengo la shirikia hilo kuandaa isha
hiyo ni kutaka kujua wanafunzi wanauwelewa gani kuhusu mambo ya Utandawazi na jinsi inavyowaathiri vijana .
Alisema katika shindano hilo walimu waliwashirikisha
wanafunzi wao , ambapo mambo mengi yalibainika kuhusu vijana kuelewa vizuri
athari za utandawazi kwa jamii hii ya kizazi kipya kama matumizi ya Internet ,
simu na mambo mengine mengi.
Katika shindno hilo mwanafunzi Faiza Khanis Ussi wa kidato
cha tatu kutoka shule ya Sunni Madressa toka Zanzibar aliibuka kuwa mshindi wa kwanza kwa kupata
alama 81 ambapo alizawadiwa Laptop moja
aina HP na Certificate , mshindi wa pili ni Maulid Juma kidato cha tatu toka
Kibaha secondary alipata alama 77
alipatiwa music system na mshindi wa
tatu ni Winfrida Leonard kidato cha tatu
toka WamaNakayama alipata alama 68 naye
alipatiwa zawadi music system na wanafunzi wengine wote walipatiwa zawadi
mbalimbali kwa wale walioshiriki zoezi hilo.
Akikabidhi zawadi hizo Afisa elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Bw. Raymond Mapunda alisema JATA imetoa hamasa kubwa kwa vijana katika kuwapiwa
uwezo wao juu ya uelewa wao katika utandawazi .
Alisema kama wanafunzi wakiwa makini kwa mambo ya utandawazi
kwa kuepuka matumizi mabaya wanaweza kufanya vizuri katika masomo yao lakini
kama wakitumia vibaya yatawasababishia madhara
makubwa.
No comments:
Post a Comment