PCHA ZA MSIBA WA GOLDIE MUME WAKE PAMOJA NA WENGINE WALIOHUDHURIA
    
    
    
    
Wa
 pili kutoka kushoto ni mtangazaji wa Channel O Denrele Edun ambae 
alikua rafiki mkubwa wa Goldie na ndioGoldie alifia mikononi mwake akiwa
 amembeba, huu msiba ulihudhuriwa na watu wachache walioalikwa tu huko 
Ikoyi Lagos Nigeria.
Gazeti la Daily Post liliripoti
 leo asubuhi kwamba msanii Goldie ambae aliiwakilisha Nigeria kwenye 
jumba la Big Brother 2012 anazikwa leo, baada ya muda kupita ndio 
nimezipata hizi picha za msiba wa Goldie ambae alifariki siku ya 
Valentine feb 14 2013.
Imeripotiwa kwamba manenoya 
mwisho ya Goldie yalikua ni kumuomba baba yake amuombee apone maumivu 
makali ya kichwa aliyokua nayo ambapo Daily Post wameripoti tena kwamba 
staa huyo alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali, foleni ya magari 
siku hiyo ya wapendanao ilichangia kuchelewa kufika hospitali.
Chanzo mojawapo cha kifo chake ni shinikizo la damu na maradhi ya moyo.















No comments:
Post a Comment