LONDON FASHION WEEK TANZANIA IMO YA KUMI BORA
Nje ya
Jumba la Somerset- Samson Soboye (Mpangaji wa maonyesho), Jacqueline
Kibacha ("Heart 365"), Mama Balozi Joyce Kallaghe, Anna Lukindo ("Anna
Luks") na Rose Kiondo (Mratibu wa maonyesho)
Wanamitindo
wa Kitanzania kwenye London Fashion Week 2013. Anna Lukindo, Christine
Mhando, Jacquiline Kibacha-pic by Urban Pulse"
Jumapili
mchana wilaya ya Westminster jijini London ilikuwa na mashindano ya
ubunifu na urembo katika maonyesho ya kimataifa ya London Fashion Week.
Mashindano haya yalifanyika jumba la Somerset lililosimama imara
kwenye upembe wa kaskazi ya mto Thames.
toka
tarehe 14 hadi tarehe 28. Wiki hizi mbili nzima zitakutanisha kila mtu
anaye husika na biashara ya mavazi na urembo. Magwiji na mapapa wa
mitindo, wabunifu, walimbwende, watafuta vipaji, wafanya biashara,
wazalishaji mali ghafi na wamiliki viwanda. Wote hukutana katika
maonyesho haya. Hapa si vipaji tu vinavyojionyesha, bali pia watu wa
biashara.
Siku hii
Tanzania ilikuwa moja ya nchi mbili tu za Kiafrika zilizochaguliwa na
British Council na "London Fashion Week" kushiriki mashindano ya
kutafuta vipaji chipukizi kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi na urembo.
Watanzania Anna Lukindo, Jacqueline Kibacha na Christine Mhando ndio
wasanii waliobeba bendera ya taifa letu na kutuwakilisha katika
mashindano haya ya kimataifa yanayofanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka
27 sas
No comments:
Post a Comment