Zitto Kabwe kuhusu usalama wake.. wakati mgumu kwake kisiasa.. Ana hizi sentensi nyingine 11
Ni mengi ambayo yamesikika kuhusu Mbunge Zitto Kabwe
siku za hivi karibuni, mojawapo ni ishu ya Mbunge huyo kusimamishwa
Uanachama wa CHADEMA na pia akaamua kwenda kuongea na Wapigakura wake
kwamba hatogombea tena nafasi hiyo.
Huenda kuna vitu hukuwahi kumsikia akizungumzia, mojawapo ni ishu ya usalama wake; “Suala
la usalama sina tatizo kabisa kwa sababu ninachokifanya ni majukumu ya
Kikatiba.. Wananchi wanachagua kundi la Wabunge 350 kwa ajili ya kazi
tatu.. uwakilishi, kutunga Sheria na kuisimamia Serikali.. Hamjawahi
kunisikia nalalamika kuhusu usalama, likitokea limetokea huwezi jua
binadamu wanapanga nini…”
Zitto Kabwe anazungumzia miaka miwili ambayo ilikuwa migumu sana kwake kwenye siasa; “Kwanza 2007 wakati nimetoa hoja ya BUZWAGI..
Kipindi kile ilikuwa ni vigumu sana kwa Mbunge kusimama na kumwambia
Waziri wa Serikali kamba umesema uongo.. Nikasimamishwa Ubunge kwa miezi
minne..“
2014
pia ulikuwa ni mwaka mgumu na una sababu mbalimbali. Kwa mara ya kwanza
nilijikuta nakwenda Mahakamani kwa ajili ya kutetea haki yangu kuhusiana
na uanachama wangu kwenye chama.. Lakini ndio mwaka huo huo ambao
nikawa na hoja nzito sana kwenye Bunge, hoja ya Escrow..“– Zitto KABWE.
Hii ni sehemu ya mahojiiano ya Mbunge huyo kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITV kilichoruka leo March 16.
No comments:
Post a Comment