Necta yasogeza muda usajili wa watahiniwa
BARAZA la
Mitihani la Tanzania (Necta) limesogeza muda wa kujisajili kwa
watahiniwa wa kujitegemea kwa ajili ya mtihani wa kidato cha nne.
Akizungumza
na HabariLeo, Ofisa Habari wa Necta, John Nchimbi alisema hatua ya
kusongeza mbele muda huo ni kutoa nafasi kwa watahiniwa kutafakari na
kufikia uamuzi wa kufanya mtihani.
Alisema watahiniwa wa kujitegemea wamepewa muda wa kujisajili hadi Machi 31 mwaka huu, ambapo watasajiliwa bila kulipa faini.
Watahiniwa
watakaojisajili katika kipindi cha kawaida watalipa ada ya Sh 50,000
kwa wanaojisajili mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Sh 30,000 kwa
wanaojisajili mtihani wa Maarifa (QT).
Awali,
NECTA iliweka hadi Februari 28 mwaka huu kwa watahiniwa kujisajili kwa
ajili ya mtihani wa Kidato cha Nne na Maarifa bila faini, kabla baraza
hilo kuongeza mwezi mmoja wa watahiniwa wa kujitegemea.
Nchimbi
alisema baada ya muda huo kupita, dirisha la usajili kwa ajili ya
watahiniwa wa kujitegemea litakuwa wazi hadi Aprili 30, lakini
watahaniwa watatakiwa kulipa na faini.
Aidha,
Nchimbi aliwataka waombaji wote kuhakikisha kujisajili kwa njia ya
mtandao kupitia tovuti ya Necta ya www.necta.go.tz na kuwa kabla ya
kufanya hivyo wanatakiwa kwenda kwenye vituo wanavyokusudia kufanyia
mtihani kuchukua namba rejea ambazo zinatolewa bila malipo.CHANZO:HABARI LEO
No comments:
Post a Comment