Kunyonyesha muda mrefu ni faida?
Utafiti
uliofanyika nchini Brazil umebaini kuwa watoto wanaonyonya kwa muda
mrefu wanakuwa na akili zaidi,wasomi,na wenye uwezo kifedha wanapokuwa
watu wazima.
Ripoti ya
utafiti huo iliyochapishwa katika jarida la afya la Lancet Global
Health unafuatilia makuzi ya mtoto hadi kuikia utu uzima wake.
Wataalam
hao wanasema kwa mtoto anayenyonya kwa takriban mwaka mmoja anakuwa na
kiwango cha akili cha juu zaidi ya yule ambaye hajanyonya kwa muda huo
kwa kiwango cha IQ cha mara nne zaidi.
Katika
maziwa ya mama kwa mjibu wa wataalam hao kuna madini mhimu ambayo
husaidia ukuaji wa ubongo na kuongeza kiwango cha ufahamu.
Hata
hivyo utafiti wa safari hii kwa mjibu wa wataalam hao nikwamba una
uhakika zaidi kwani walitumia kubwa ya watoto tofauti na idadi
iliyotumika awali miaka 1980.CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment