Airbus A320 : Hollande, Merkel na Rajoy kwenye eneo la tukio
Angela
Merkel, François Hollande na Mariano Rajoy wakiwasili kwenye eneo la
tukio katika mlima wa Alpes, Jumatano Machi 25 mwaka 2015
Na RFI
Operesheni
kubwa imerudi kufanyika Jumatano wiki hii katika mlima wa Alpes kusini
mwa Ufaransa, katika jaribio la kupata miili 150 ya watu waliofariki
katika ajali ya Airbus A320 ya shirika la ndege la Ujerumani la
Germanwings iliyoanguka Jumanne wiki hii.
Kisanduku
cheusi cha kurekodi mawasiliano katika ndege kiliyookotwa kimeanza
kufanyiwa uchunguzi mjini Paris, nchini Ufaransa na matokeo ya awali
yalikua yanatazamiwa kutolewa alaasiri Jumatano wiki hii.(P.T)
Rais wa
Ufaransa François Hollande, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri
mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy wamewasili kwenye eneo la tukio.
Viongozi
hao wamekutana na madaktari, maafisa wa Idara ya huduma za dharura na
wanajeshi ambao wanaendelea na zoezi la kutafuta miili ya wahanga. Miili
ya raia wawili kutoka Uhispania imetambuliwa miongoni mwa abiria.
Kisanduku
hicho cha sauti kiliyopatikana ni kile kinachorekodi sauti ya marubani
na maafisa wanaowasiliana nao kwenye viwanja vya ndege. Licha ya kuwa
kisanduku hiki kimeharibika, kimesafirishwa mapema asubuhi Jumatano wiki
hii kwenye Ofisi ya Uchunguzi na Uchambuzi (BEA) mjini Paris.
No comments:
Post a Comment