Daraja linalolalamikiwa na wakazi wa eneo la Kivule jijini Dar.
Watembea kwa miguu pamoja na gari wakionekana kupita katika daraja hilo.
Mwonekano wa daraja hilo.
WATUMIAJI
wa Barabara ya Kivule jijini Dar, wameilalalamikia serikali kwa
kushindwa kutengeneza Daraja la Kerezange maarufu ‘Silali’ ambalo
limekuwa kero kwa wakazi wa eneo hilo kufuatia mvua zinazoendelea
kunyesha ambazo zimesababisha daraja hilo kukaribia kukatika.(P.T)
Mwanahabari
wetu alifanikiwa kuongea na baadhi ya raia wanaolitumia daraja hilo
ambapo walisema kuwa kipindi hiki cha mvua maji huwa yanajaa mpaka juu
ya daraja na kusababisha kushindwa kuvuka hali inayopelekea kukwamisha
shughuli zao.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Kivule-Ukonga, Waitara Mwita Mwikwabe, alisema
kuwa tatizo la daraja hilo ni la muda mrefu kwani hata mwaka jana kuna
tukio la mtu kufariki katika mto huo baada ya kutumbukia wakati maji
yalipokuwa yamefunika daraja zima huku yeye akiwa anajaribu kuvuka.
Alisema
kuwa Manispa ya Ilala inatambua tatizo hilo na iliwahi kupeleka
mkandarasi kwa ajili ya kulitengeneza lakini cha kushangaza tangu
alipoenda kulitazama hakurudi tena.
Alizidi
kueleza kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Ilala ilisema katika kipindi cha
mwaka wa fedha wa 2014/2015 chini ya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli
kuwa barabara ya eneo hilo pamoja na daraja hilo vingetengenezwa lakini
mpaka sasa hakuna kilichofanyika.
No comments:
Post a Comment