TIFFAN ENT

TIFFAN ENT

TUKO WANGAPI

TUKO WANGAPI

GLORY FREIGHT

GLORY FREIGHT

Wednesday, March 18, 2015

Hiki alichokifanya kuutoa ujauzito wa mpenzi wake ni ishu ambayo imechukua headlines !

woman-holding-cocktail-glass-bar 
Mwanaume mmoja Norway anashikiliwa kwa tuhuma za kumsababishia majeraha mpenzi wake pamoja na kumtoa ujauzito bila ridhaa yake, baada ya kumuwekea vidonge kwenye kinywaji na kusababisha ujauzito wake kuharibika.
Jamaa huyo alifanya ukatili huo baada ya kumuwekea mpenzi wake vidonge ya kutoa mimba kwenye kinywaji alichokuwa anakunywa kwa lengo la kumtoa ujauzito wa miezi minne aliokuwa nao, ambapo alifikia hatua hiyo baada ya kumshawishi kuutoa kwa muda mrefu bila mafanikio.
Mwanamke huyo amesema mpenzi wake alikuwa akimshawishi mara nyingi kutoa ujauzito huo lakini hakukubaliana nae, baada ya kunywa kinywaji hicho alihisi maumivu makali ya tumbo na alipoenda Hospitali kufanyiwa vipimo ilionekana ujauzito wake umeharibika tayari.
Hata hivyo mtuhumiwa huyo alikiri kufanya kosa hilo na kusema anajisikia vibaya, amefanya hivyo kwa sababu ilikuwa njia pekee ya kufanikisha lengo lake kuutoa ujauzito huo, Mahakama imemhukumu kifungo cha miaka saba jela

No comments:

Post a Comment