Boko Haram: wanajeshi wa kikosi cha muungano wadhibiti Damasak
Wanajeshi wa Chad wakipiga doria katika ardhi ya Nigeria dhidi ya Boko Haram, Februari 3 mwaka 2015.
Na RFI
Majeshi
ya Niger na Chad, ambao wanaendesha kwa pamoja mashambulizi tangu
Jumapili wiki iliyopita dhidi ya Boko Haram nchni Nigeria, wameuweka
chini ya udhibiti wao mji wa Damasak, uliokua mikononi mwa wanamgambo wa
Nigeria.
Mji huo unapatikana kwenye umbali wa zaidi ya kilomita mia moja na magharibi mwa pwani ya ziwa Chad.
Ni
mafanikio yakwanza katika vita hivi viliyoanzishwa dhidi ya Boko Haram.
Lakini hasara ni kubwa ikiwa ni pamoja na kuuawa kwa wanajeshi kadhaa wa
Chad na Niger.(P.T)
Kulingana
na vyanzo kadhaa, hasara ni kubwa upande wa watu waliouawa katika
mapigano hayo. Takribani wanamgambo 200 wa Boko Haram wanasadikiwa kuwa
wameuawa, na upande wa wanajeshi wa Chad wanasadikiwa kuwa 10 ni
miongoni mwa waliouawa kuhu 20 wakijeruhiwa. Chanzo kingine cha
hospitali kimebaini kwamba wanajeshi 33 wamejeruhiwa.
Kwa sasa,
hakuna taarifa yoyote kutoka upande wa serikali ya Chad na hakuna
tangazo lolote la serikali hata la jeshi la Niger kuhusiana na hasara
iliyotokea katika mapigano hayo.
Boko
Haram iliudhibiti mji wa Damasak Novemba 24 mwaka 2014 na iliwaua watu
zaidi ya hamsini na kusababisha wengine 3000 kuyahama makazi yao, kwa
mujibu wa Ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi.
Wakati huu wanamgambo wa Boko Haram walipenya na kuingia katika mji huo kama wafanyabiashara, huku wakificha silaha zao.
No comments:
Post a Comment