Burundi:Hussein Rajabu azungumza na BBC
Hussein Rajabu azungumza na BBC
Aliyekuwa
mwenyekiti wa chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD Hussein Rajabu
aliyekuwa ameripotiwa kutoroka jela amemlaumu rais Pierre Nkurunziza kwa
kumpangia njama ya kumfunga jela ilikutokomeza demokrasia nchini humo.
Bwana
Rajabu ameiambia BBC kuwa yeye yuko salama na wala hakutoroka jela kama
ilivyodhaniwa bali kuwa alitoka jela ''rasmi''baada ya kushirikiana na
wafuasi wa chama chake.
Rajabu amesema kuwa wazalendo wenza wa CNDD-FDD ndio walifanikisha kuondoka kwake gerezani kwa ''heshima na taadhima''.
Aidha
amemlaumu rais Nkurunziza kwa kukiuka mkataba wa Arusha na badala yake
kuunda jopo la wazee aliloliita ''Baraza la Busara'' kwa nia ya
kutenganisha viongozi wengine wa chama hicho cha CNDD-FDD(BBC)
''nimekuwa
nikisubiri warundi wenzangu wajadili hili swala wenyewe na pia kwa
ushirikiano na viongozi wa mataifa ya kigeni kwa niya ya kutafuta
suluahu.''
''kila mtu anajua kuwa sikuwa na hatia yeyote .
''mimi ndiye mwanasiasa aliyepewa adhabu kali zaidi hata ikilinganishwa na watu waliotenda makosa makubwa zaidi ya yangu''
''Ni wazi
kuwa ndugu rais Pierre Nkurunziza hakuridhika na majukumu na mapato
aliyokuwa nayo na hivyo akanidhulumu'' alisema Bwana rajab.
Hussein Rajabu alikuwa mwanasiasa mashuhuri nchini humo alipohukumiwa kifungo cha miaka 13 jela, mwaka 2007.
Bwana Rajabu alishitakiwa kwa kutaka kuzua vurugu nchini.
Kabla
akamatwe mwaka 2007 Hussein Rajabu alikuwa mshirika wa karibu wa rais wa
Burundi Pierre Nkurunziza na mwenyekiti wa chama tawala.
No comments:
Post a Comment